Kama una nywele zako zinanyonyoka, usi panic labdaulikuwa hujui tatizo
basi fuatana nami . Sababu inaweza kuwa rahisi. Inaweza kuwa ni ukosefu wa vitamin au sababu za kinasaba ( urithi ).
1. Stress
Kila aina ya physical and emotional pain inaweza kusababisha kunyonyoka kwa nywele. Ajali ya gari au kufanyiwa upasuaji vinaweza kukusababishia stress ambayo itakuletea kunyonyoka kwa nywele zako.
Emotional stress hazisababishi kunyonyoka kwa nywele lakini inaweza kutokea pale unapokuwa katika wakati mgumu kisaikolojia kama vile kumpoteza mtu wako wa karibu kutokana na kifo au kuachwa kimapenzi. Hata hivyo,. Baada ya wakati huo mgumu, nywele zako zitaanza kuota tena baada ya miezi sita.
2. Homoni
Kunyonyoka kwa nywele kunaweza kuwatokea wanawake w alio katika menopause kutokana na kuadilika kwa viwango vya homoni. Inaweza kutokea pia kwa wanawake wanaotumia
vidonge vya uzazi wa mpango hususani wanapokuwa wana ahirisha mara kwa mara zoezi la kutumia vidonge hivyo. Unashauriwa kama unatumia vidonge kwa uzazi wa mpango, basi hakikisha unazingatia ratiba na usiahirishe hata mara moja.
3. Ukosefu wa Protini au Hamirojo
Ukosefu wa protini unaweza kudhoofisha ukuaji wa nywele au kusababisha kunyonyoka kwa nywele kabisa na hatimaye kuwa na kipara kabisa.
4. Ujauzito
Ujauzito ni miongoni mwa mambo yanayo leta physical stresses and there are also na pia huleta mabadiliko ya homoni. Kunyonyoka kwa nywele hutokea baada ya kujifungua.
Kama mmoja kati ya wazazi wako au babu zako wa upande wa baba au mama aliwahi kuwa na tatizo la kunyonyoka nywele au kuwa na kipara kabisa, basi kuna uwezekano mkubwa sana kwa jambo hilo kutokea kwako pia kwa sababu za urithi.
Hakuna maelezo yoyote ya kitabu kuhusu jinsi ya kukinga suala hili , hata hivyo unaweza kujaribu kutumia vyakula na dawa mbalimbali bila kujali sababu iliyo fanya unyonyoke nywele au kuwa na kipara.
6. Vinasaba vya kiume
Tafiti mbalimbali za kisayansi zinaonyesha kuwa, wanaume wengi wana anza kuonyesha dalili za kunyonyoka mwele wakiwa na umri wa kuanzia miaka sitini ( 60) na kuendelea.
So kama wewe ni mwanaume mwenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea na nywele zako zimeanza kuonyesha dalili za kunyonyoka, huna haja ya kupanic wala kutafuta tiba, kwani suala hilo ni la kawaida kabisa kwa wanaume wenye umri wako.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.