Wasichana wanaoolewa wakiwa wadogo mara nyingi huwa hawawezi kuendelea na masomo, mara nyingi hudhulumiwa na waume zao, kupigwa na hata kunyanyaswa kingono. Hupachikwa mimba na pia huwa hatarini ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ukiwemo Ukimwi.
Ripoti hiyo iliyopewa jina Every Last Girl, imeorodhesha nchi ambazo ni ngumu zaidi kwa wasichana baada ya kuzingatia elimu, ndoa za watoto, mimba za mapema, vifo vya wanawake wakijifungua na idadi ya wanawake bungeni.