Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pia kumbuka, Desemba ndiyo kipindi ambacho kampuni za simu na fanicha zinafanya promosheni za bidhaa zao. Kwa hiyo utake usitake, ukiingia kwenye uhusiano mpya kwa kipindi hiki, hakikisha umeandaa hela ya kumnunulia mtu ‘smartphone’ mpya na ‘dressing table’ fulani hizi ya bei mbaya
 
Kwa kifupi, kama unataka kuzitumia pesa zako kwa amani ndani ya mwezi huu hakiksha hujiingizi kwenye uhusiano mpya na mwanamke wa mjini – ngoja ngoja kwanza mambo yatulie, mwanzoni mwa 2018 tutaambiana tuendelee na kazi zetu hali ya hewa ikitulia.
 
Rais John Magufuli amevunja rekodi kwqa kusamehe wafungwa 8,157 ikiwamo familia ya mwanamuziki wa dansi Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ jana Jumamosi.
 
Liverpool watakuwa nyumbani huko Anfield leo kuwakaribisha Everton mechi itakayopigwa saa kumi na moja na robo (11:15 jioni).

Timu hizo zinakwenda kwenye mechi hiyo kila moja ikiwa katika hali nzuri baada ya kushinda mechi zao zilizopita, ambapo Everton ilishinda mabao matatu ugenini kwenye Europa League, huku Liverpool ikimpiga mtu mabao saba kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mechi nyingine ya leo, Arsenal iliyoshinda BATE 6-0 watakuwa na shughuli pevu ugenini kwa Southampton.
 
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amewataka wachezaji wake kuepuka mipira ya adhabu karibu na goli lao na kutopaki basi wakati watakapowakabili watani zao wa jadi Manchester United kwenye Uwanja wa Old Trafford leo Jumapili.

Guardiola amewaonya wachezaji wake kuacha kutengeneza mazingira ya mipira ya adhabu katika mchezo huo muhimu zaidi kwao.
 
Kocha huyo Mhispania, anahofia Man United inaweza kupata mabao kupitia mipira ya adhabu endapo Man City haitakuwa makini.

Man United ina wachezaji wengi warefu kulinganisha na Man City. Romelu Lukaku, Nemanja Matic, Chris Smalling na Zlatan Ibrahimovic ni wachezaji warefu ambao watakuwa tishio kwa Man City.
 
Kiungo wa pembeni aliyerudishwa kucheza beki wa kushoto Ashley Young amepata umaarufu kwa mashuti ya mpira wa adhabu.

Inakadiriwa kuwa watu zaidi ya bilioni moja watakuwa wakitazama pambano la Manchester United dhidi ya Manchester City.
 
Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba ataukosa mchezo huo akitumikia adhabu yake ya kufungiwa mechi tatu baada kuonyeshwa kadi nyekundu katika pambano lililopita dhidi ya Arsenal baada ya kumkanyaga mlinzi wa kulia, Hector Bellerin na pia atazikosa mechi dhidi ya Bournemouth na West Brom.

Wengine watatu watakaokosa mechi hiyo ni mabeki watatu, John Stones na Benjamin Mendy wa Manchester City na Eric Baily wa Manchester United wote hawa ni majeruhi.
 
Back
Top Bottom