Bendera pia amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Mbali ya ukuu wa mkoa, amewahi kuwa mbunge wa Korogwe Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo katika utawala uliopita wa Rais mstaafu, Kikwete.
Bendera pia amewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Mbali ya ukuu wa mkoa, amewahi kuwa mbunge wa Korogwe Mjini na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo katika utawala uliopita wa Rais mstaafu, Kikwete.
Serikali inashirikiana na Umoja wa Mataifa (UN) kuhakikisha miili ya askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa na waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inarejeshwa nchini.
Akizungumzia na waandishi wa habari leo Jumapili Desemba 10, 2017 Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali James Mwakibolwa amesema miili ya askari hao itarejeshwa nchini kati ya Jumanne Desemba 12, au Jumatano Desemba 13,2017.
Mwakibolwa amesema tukio hilo lililotokea Desemba 7,2017 katika kambi ndogo iliyopo katika daraja la Mto Simulike, kaskazini mashariki mwa Wilaya ya Beni, Jimbo la Kivu.
Taratibu za kusafirisha miili ya marehemu kuirejesha nchini inafanyika chini ya uratibu wa Serikali na Umoja wa Mataifa. JWTZ na Serikali tunaendelea kuchukua hatua stahiki kufuatilia tukio hili ikiwemo kufanya uchunguzi katika eneo husika," amesema Mwakibolwa.
Amesema tukio hilo halitawavunja moyo JWTZ wala kutetereka kupeperusha bendera ya Tanzania ndani na nje ya nchi bali linawaongezea ari, nguvu, ushupavu na uhodari zaidi katika kutekeleza majukumu yao.
Ni bahati mbaya mashujaa wetu wameuawa wakiwa wanatekeleza jukumu la ulinzi wa amani nchini DRC. Kwa umoja wetu Watanzania tuwaombee dua roho zao zipumzike kwa amani na majeruhi wapone haraka iwezekanavyo ili warejee kutekeleza majukumu yao," amesema.
Mvua ilinyesha usiku wa kuamkia jana Jumamosi Desemba 9,2017 saa nane usiku pasipo kukata hadi saa kumi na moja jioni. Mvua ilikata kwa muda na kuendelea kunyesha usiku hadi leo Jumapili Desemba 10,2017.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.