Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

SHAW ADAI MALIPO ILI AKUBALI KUONDOKA UNITED


Luke Shaw atakubali kuondoka Manchester United ikiwa klabu hiyo itamlipa paundi milioni 5 kufidia hasara za mapato yake, kwa mujibu wa = Sun .
Mchezaji huyo asiyepewa nafasi chini ya uongozi wa Jose Mourinho, anatarajiwa kuwekwa sokoni Januari. Akiwa hawezi kudai kulipwa ujira kama anaopokea Old Trafford kwa klabu nyingine, Shaw ataidai United kufidia kiasi kitakachopungua kabla ya kuondoka.
 
BAYERN YAMTENGEA DAU LENO


Bayern Munich wamemfanya nyota wa Bayer Leverkusen Bernd Leno kuwa shabaha yao kuu katika dirisha la uhamisho wa Januari kwa mujibu wa Bild .
Mjerumani huyo anaonekana kama mbadala sahihi wa Manuel Neuer kwani mkongwe huyo anasumbuliwa na majeraha ya mguu.
 
COUTINHO KUMALIZIA MSIMU HUU ANFIELD


Philippe Coutinho wa Liverpool yupo tayari kusubiri hadi mwisho wa msimu kujiunga na klabu ya Barcelona, kwa mujibu wa Daily Mirror .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili anatamani kutua Camp Nou kucheza pamoja na Lionel Messi, lakini analazimika kubaki Anfield kwani Liverpool hawatakuwa tayari kumruhusu kuondoka dirisha la uhamisho wa Januari badala yake ataondoka majira ya joto.
 
COUTINHO KUMALIZIA MSIMU HUU ANFIELD


Philippe Coutinho wa Liverpool yupo tayari kusubiri hadi mwisho wa msimu kujiunga na klabu ya Barcelona, kwa mujibu wa Daily Mirror .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili anatamani kutua Camp Nou kucheza pamoja na Lionel Messi, lakini analazimika kubaki Anfield kwani Liverpool hawatakuwa tayari kumruhusu kuondoka dirisha la uhamisho wa Januari badala yake ataondoka majira ya joto.
 
MAN UTD WANAMTAKA KINDA WA WHITECAPS


Manchester United wamemwalika kinda wa Vancouver Whitecaps Alphonso Davies kufanya majaribio Januari kwa mujibu wa CTV Edmonton .
Kinda huyo wa miaka 17 ambaye amekuwa mchezaji mdogo zaidi kuichezea timu ya taifa ya Canada majira ya joto, anasubiri kupata kibali kutoka kwenye klabu yake kutua United.
 
MAN CITY NA LIVERPOOL ZAMWANIA SERI


Manchester City na Liverpool zinapambana kuipata saini ya kiungo wa Nice Jean Michael Seri, kwa mujibu wa Daily Mail .
Muaivory Cost huyo alihusishwa na tetesi za kutaka kutua Barcelona majira ya joto, lakini kwa sasa yupo tayari kutua Uingereza.
 
ARSENAL YAKARIBIA KUMSAJILI GORETZKA


Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa kiungo wa Schalke Leon Goretzka na watampata kama mchezaji huru, kwa mujibu wa The Sun .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani atakuwa amemaliza mkataba wake mwisho wa msimu huu na yupo huru kuzungumza na klabu nyingine Januari, Arsenal nao wakiwa kwenye foleni.
 
REAL YAANZA MAZUNGUMZO NA HAZARD


Real Madrid wamewasiliana na mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard kuangalia uwezekano wa kumleta Mbelgiji huyo Hispania kwa mujibu wa Diario Gol .
Mchezaji huyo anasita kusaini mkataba mpya Stamford Bridge na ameeleza jinsi anavyoihusudu Real Madrid.
 
INTER YAPIGANA VIKUMBO NA JUVE KUMSAJILI CAN


Inter wapo tayari kupigana vikumbo na Juventus kwa ajili ya saini ya mchezaji wa Liverpool Emre Can, kwa mujibu wa Tuttosport .
Kiungo huyo atakuwa amemaliza mkataba wake Anfield mwisho wa msimu huu na alikuwa karibu kutua Turin majira ya joto.
 
CHELSEA YAMTENGEA £20M BAILEY


Chelsea wapo tayari kutoa kitita cha paundi milioni 20 kwa ajili ya winga wa Bayer Leverkusen Leon Bailey, limedai The Sun .
Blues wamekuwa wakimfuatilia Mjamaica huyo kwa kipindi cha miezi 18 na wanataka kuipiku Barcelona kumsajili mchezaji huyo wa miaka 20.
 
BETIS WANATAKA KUMSAJILI STURRIDGE


Real Betis wanaandaa ofa kumsajili Daniel Sturridge kutoka Liverpool, kwa mujibu wa El Gol Digital .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekuwa akihaha kutafuta muda wa kucheza zaidi Anfield na atapewa nafasi kutimkia Hispania Januari.
 
MAN UTD KUMUUZA SHAW & DARMIAN


Manchester United wapo tayari kusikiliza ofa kuwauza mabeki wao Luke Shaw na Matteo Darmian, kwa mujibu wa The Daily Record .
Shaw ambaye amesumbuliwa na majeraha amepewa nafasi kujiunga na klabu nyingi za Uingereza wakati Muitaliano Darmian hatakiwi kwenye kikosi cha Jose Mourinho.
United wanataka kutunisha mfuko wao ili kuwasajili beki wa kushoto Alex Sandro na Danny Rose majira ya baridi.
 
MAN UTD YATENGA DAU KUMSAJILI ASENSIO


Manchester United itafanya mchakato kumsajili kiungo wa Real Madrid Marco Asensio dirisha la uhamisho la Januari baada ya kuachana na mpango wa kumsajili Gareth Bale, kwa mujibu wa Don Balon .
Mashetani Wekundu wanajiamini watafanikiwa kumsajili mchezaji huyo wa miaka 21 kwani ameshindwa kupata nafasi ya kudumu Santiago Bernabeu.
 
BATSHUAYI HURU KUONDOKA CHELSEA


Chelsea wapo tayari kumruhusu Michy Batshuayi kuondoka kwa mkopo kwani wanataka kusajili mshambuliaji mpya, kwa mujibu wa The Sun .
Mbelgiji huyo amekuwana wakati mgumu katika kipindi chote Stamford Bridge na ataondolewa kuachia nafasi kwenye kikosi cha Antonio Conte.
 
GIROUD ASHINIKIZA KUONDOKA KWA MKOPO


Olivier Giroud anataka kuondoka Arsenal kujiunga na klabu nyingine kwa uhamisho wa mkopo, kwa mujibu wa Daily Mirror .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa anahitaji muda zaidi wa kucheza kujihakikishia nafasi Kombe la Dunia 2018 na amezipa angalizo Crystal Palace na West Ham.
 
UTD YATENGA £95M KUMPATA NYOTA WA LAZIO


Manchester United wanataka kuvunja rekodi yao ya usajili kwa kuinasa saini ya nyota wa Lazio Sergej Milinkovic-Savic kwa dau la £95m, kwa mujibu wa The Express .
Kiungo huyo yumo kwenye rada za miamba wa Serie A Juventus, lakini Jose Mourinho amemfanya kuwa shabaha kuu kwa bodi ya Old Trafford.
 
MAN UTD BADO WANAMTAKA PERISIC


Manchester United bado wanaitamani huduma ya Ivan Perisic baada ya kumkosa winga huyo wa Inter uhamisho wa majira ya joto, kwa mujibu wa The Sun .
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia alisaini mkataba mpya kubaki Italia, lakini mchakato huo ulifanyika kutunza thamani yake ila anaweza kupatikana Januari kwa dau la £45 milioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…