Utafiti mwingine uliofanywa na chuo kikuu cha India cha Purdue umebainisha kuwa, sumu kali inayotokana na sumu ya risasi, inayoweza kuiingia mwilini mwa binadamu kutokana na kula vitu vilivyoingiwa na sumu hiyo,
Vilevile tamaduni, mila na desturi za jamii na jinsi watu wanavyozithamini itikadi hizo, zina mafasi kubwa katika afya zao ingawa matokeo yake huweza kuwa mazuri au mabaya
Kwa mfano mazoea na mila ya kuwakeketa au kuwatahiri watoto wa kike na wanawake ina madhara makubwa kama vile kuongeza kiwango cha maambukizo ya magonjwa na hata matatizo ya kiakili miongoni mwa wasichama na wanawake wanaofanyiwa jambo hilo.
Utafiti uliochapishwa katika Jarida la Afya ya Jamii na Elimu ya Magonjwa ya Mlipuko umebainisha kuwa, wakati vijana wanapovaa mavazi kwa mujibu wa mila na tamaduni za makundi au makabila yao, suala hilo huweza kuwapunguzia uwezekano wa kupatwa na matatizo ya kiakili baadaye maishani.
Urithi wa jenetiki ni suala jingine linaloathiri afya za watu. Kuishi muda mrefu, siha ya mwili kwa ujumla na kupatwa na baadhi ya magonjwa na hata kuzaliwa nayo, ni masuala yanayoainishwa na jinsi jeni zetu zilivyo mwilini tangu wakati tunapozaliwa.
Mambo mengine ni pamoja na vyakula tunavyokula, harakati zetu kifizikia, tabia na mazoea tofauti kama kuvuta sigara au kunywa pombe na kutumia madawa ya kulevya. Pia jinsi tunavyoweza kuvumilia mfadhaiko wa kifikra au stress yote hayo yana nafasi muhimu katika uzima wetu kimwili na kiakili.
Suala jingine tunaloweza kulitaja hapa ni matumizi ya vituo vya afya na hospitali. Jamii ambayo ina vituo vya afya vya kutosha, vilivyo vizuri na vyenye kukidhi mahitaji ya watu wa jamii hiyo, watu wake wana nafasi zaidi ya kuwa na siha nzuri kuliko jamii au watu wanaoishi maeneo ambayo hayana vituo vya afya au hospitali.
Kwa mfano nchi zilizoendelea zenye vituo vya afya na hospitali za kutosha na nzuri, watu wa nchi hizo huishi maisha marefu zaidi ikilinganishwa na nchi masikini zenye upungufu katika sekta hiyo.
Jinsia ya mtu pia huathiri afya yake. Kuna magonjwa yanayowapata wanawake zaidi na kuna magonjwa yanayowapata wanaume zaidi. Hali ya miili ya wanawake hutofautiana na wanaume na hata kazi na shughuli wanazozifanya pia huweza kuathiri afya zao kwa ujumla.
Kwa mfano, kubeba mimba na kujifungua, kansa ya ovari na kizazi huathiri afya ya wanawake katika hali ambayo wanaume hupatwa na kansa ya tezi kibofu na ya korodani. Wakati wa vita wanaume hushiriki kwa wingi kuliko wanawake na matokeo yake ni kuuawa au kujeruhiwa.
Wanawake na wasichana huenda wakawa wahanga wa vitendo vya utumiaji mabavu dhidi yao na ukatili kuliko watoto wa kiume na wanaume. Katika baadhi ya jamii watoto wa kike na wanawake huwa hawapewi fursa ya kupata elimu na kujiendeleza kama wanaume, suala ambalo huathiri afya zao pia. Tafiti nyingi zimeonyesha ubaguzi wa kijinsia katika utoaji huduma za afya hata katika nchi zilizoendelea.
Wanawake na wasichana huenda wakawa wahanga wa vitendo vya utumiaji mabavu dhidi yao na ukatili kuliko watoto wa kiume na wanaume. Katika baadhi ya jamii watoto wa kike na wanawake huwa hawapewi fursa ya kupata elimu na kujiendeleza kama wanaume, suala ambalo huathiri afya zao pia. Tafiti nyingi zimeonyesha ubaguzi wa kijinsia katika utoaji huduma za afya hata katika nchi zilizoendelea.
Miongoni mwa mambo muhimu yanayoijenga afya ya mwanadamu ni kula lishe salama na mlo uliokamilika. Tunaposema lishe salama na mlo uliokamilika au healthy balanced diet kwa kimombo, tunamaanisha masuala muhimu mawili.
Moja ni kula kiwango kinachotakiwa cha chakula kwa mujibu wa harakati na hitajio la mwili wako, na pili ni kula aina tofauti za vyakula vinavyotakiwa ili kuijenga siha ya mwili. Tunapaswa kufahamu kwamba, kula lishe bora ni suala muhimu linalochangia kuimarisha afya ya mwili.
Lishe salama na iliyokami inamaanisha kula vyakula tofauti kutoka katika mafungu manne makuu ya vyakula na kupunguza baadhi ya vyakula katika milo tunayokula kila siku.