Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ufuatao ni ushauri au vidokezo muhimu (tips) kuhusiana na namna ya kula vyema ili kuzilinda na kuziimarisha afya zetu. Tunashauriwa mlo tunaokula uwe na kiasi cha kutosha cha wanga, kwani aina hiyo ya chakula huipa miili yetu nguvu. Tunashauriwa kula matunda na mboga kwa wingi kila siku.
 
wanapaswa kula virutubishi muhimu vinavyotupatia mada zinazopatikana kwenye samaki kwa ajili ya afya ya miili yetu. Tunashauriwa kupunguza kwa kiasi kikubwa sukari na mafuta katika milo yetu. Vilevile tunashauriwa kula chumvi kwa kiwango kidogo, isizidi gramu 6 kwa siku kwa watu wazima.
 
Tunapaswa kufahamu kuwa, baadhi ya vyakula tayari vina kiwango cha chumvi ndani yake kwani karibu theluthi moja ya chumvi katika milo yetu hutoka katika vyakula ambavyo tayari vimeshatengeneza kama supu iliyo tayari, sosi, mikate, asusa (snacks), pai, pizza vyakula vinavyosindikwa na kuhifadhiwa.
 
Hivyo kuna umuhimu wa kula vyakula hivyo kwa kiasi kidogo. Hii ni kwa sababu ongezeko la chumvi mwilini huweza kumfanya mtu apatwe na shinikizo la damu, hali ambayo huweza kusababisha ugonjwa wa moyo na kiharusi.
 
Suala jingine tunalopaswa kuzingatia ni kunywa maji ya kutosha, tunashauriwa kila siku kunywa kiasi cha gilasi 6 hadi 8 za maji au vyakula vingine vya majimaji kama juisi na kadhalika, ili kuzuia upungufu wa maji mwilini.
 
Maji yana faida nyingi na baadhi yake ni kuusaidia mwili kuondoa kwa urahisi sumu na mabaki yasiyotakiwa mwilini. Kusaidia kulainisha macho na maungio ya mwili na pia hutusaidia wakati wa kumeza.
 
Jambo jingine tunaloshauriwa ni kuupa mwili harakati, mazoezi ya mara kwa mara na kuwa na uzito unaotakiwa kiafya. Jengine ni kutoacha kula kifuangua kinywa. Tunatakiwa kustaftahi kila siku kwa sababu chakula hicho cha asubuhi huupa mwili nguvu ya kuanzia siku na huamsha utendaji kazi wa mwili kwa ajili ya siku nzima.
 
6a514dbfd03b8003d1ea1e4222838007.jpg
 
Back
Top Bottom