Aina ya vyakula vinavyopaswa kuwepo kwenye milo yetu ni pamoja na matunda na mboga kwa wingi. Kiwango cha kutosha cha wanga kama vile mkate, wali, viazi, pasta na vinginevyo na ni bora viwe vinatokana na aina mbalimbali za nafaka kamili zisiokobolewa.
Maziwa na vyakula vinavyotokana na maziwa kama mtindi na jibini. Vyakula vyenye protini kama vyama, samaki, mayai, maharagwe na vinginevyo na vilevile kiasi kidogo cha sukari , mafuta na chumvi.
ufuatao ni ushauri au vidokezo muhimu (tips) kuhusiana na namna ya kula vyema ili kuzilinda na kuziimarisha afya zetu. Tunashauriwa mlo tunaokula uwe na kiasi cha kutosha cha wanga, kwani aina hiyo ya chakula huipa miili yetu nguvu. Tunashauriwa kula matunda na mboga kwa wingi kila siku.
New Word: LUKAKU Meaning: To help your enemies succeed. e.g. After interrogation, it was discovered that the robbers have been enjoying a Lukaku from the police.
Baadhi wanasema, ni bora kula aina 5 za matunda tofauti na mboga kwa siku. Pia tunashauriwa kula samaki kwa wingi kwa uchache mara mbili kila wiki na kama hatutoweza kufanya hivyo au kwa wale ambao samaki wanawadhuru na wale wasiokula nyama
New Word: LUKAKU Meaning: To help your enemies succeed. e.g. After interrogation, it was discovered that the robbers have been enjoying a Lukaku from the police.
wanapaswa kula virutubishi muhimu vinavyotupatia mada zinazopatikana kwenye samaki kwa ajili ya afya ya miili yetu. Tunashauriwa kupunguza kwa kiasi kikubwa sukari na mafuta katika milo yetu. Vilevile tunashauriwa kula chumvi kwa kiwango kidogo, isizidi gramu 6 kwa siku kwa watu wazima.
Tunapaswa kufahamu kuwa, baadhi ya vyakula tayari vina kiwango cha chumvi ndani yake kwani karibu theluthi moja ya chumvi katika milo yetu hutoka katika vyakula ambavyo tayari vimeshatengeneza kama supu iliyo tayari, sosi, mikate, asusa (snacks), pai, pizza vyakula vinavyosindikwa na kuhifadhiwa.
Hivyo kuna umuhimu wa kula vyakula hivyo kwa kiasi kidogo. Hii ni kwa sababu ongezeko la chumvi mwilini huweza kumfanya mtu apatwe na shinikizo la damu, hali ambayo huweza kusababisha ugonjwa wa moyo na kiharusi.
Suala jingine tunalopaswa kuzingatia ni kunywa maji ya kutosha, tunashauriwa kila siku kunywa kiasi cha gilasi 6 hadi 8 za maji au vyakula vingine vya majimaji kama juisi na kadhalika, ili kuzuia upungufu wa maji mwilini.
Maji yana faida nyingi na baadhi yake ni kuusaidia mwili kuondoa kwa urahisi sumu na mabaki yasiyotakiwa mwilini. Kusaidia kulainisha macho na maungio ya mwili na pia hutusaidia wakati wa kumeza.
Jambo jingine tunaloshauriwa ni kuupa mwili harakati, mazoezi ya mara kwa mara na kuwa na uzito unaotakiwa kiafya. Jengine ni kutoacha kula kifuangua kinywa. Tunatakiwa kustaftahi kila siku kwa sababu chakula hicho cha asubuhi huupa mwili nguvu ya kuanzia siku na huamsha utendaji kazi wa mwili kwa ajili ya siku nzima.