Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

William anayetamba katika kikosi cha kwanza kwa Mtaliano Antonio Conte, alisema hana mpango wa kuhama Chelsea na amewataka mashabiki wa klabu hiku kumsapoti.

Awali, ziliibuka tetesi kuwa mchezaji huyo amekubali kutua Old Trafford katika dirisha dogo kabla ya kujitokeza hadharani kukana taarifa hiyo.

“Siku zote nimekuwa na furaha Chelsea. Naipenda sana klabu hii kwa roho moja, siwezi kuondoka naomba mashabiki watulie wanipe ushirikiano,” alisema Willian.

Willian mwenye miaka 29, alifunga bao la kwanza katika mchezo wa Ligi Kuu England walioshinda mabao 3-1 dhidi ya Huddersfield.
 
Kocha wa Manchester United, Jose Mouriho ameingia hofu ya kumpoteza libero wake Eric Bailly mwenye maumivu ya kifundo cha mguu.

Mourinho alidokeza Bailly anatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina kubaini ukubwa wa jeraha hilo ambalo linaweza kupunguza kasi ya Man United.

Man United inachuana vikali kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu dhidi ya mahasimu wake Manchester City inayoongoza kwa pointi 46.

Mourinho alisema kuwa endapo beki huyo wa kimataifa wa Ivory Coast hatapata matibabu ya kina, anaweza kupata matatizo makubwa siku za usoni.
 
Bailly aliyeumia wakati akiitumikia timu ya taifa ya Ivory Coast katika mashindano ya kimataifa, amekosa mechi nane za Man United kutokana na jeraha.

“Nadhani ana tatizo kubwa. Tunapambana ili apate matibabu ya kina, lakini tunaangalia kama anaweza kufanyiwa upasuaji baada ya kupata taarifa ya daktari,” alisema Mourinho.

Mourinho alisema hawezi kutabiri kama beki huyo anaweza kukosa mechi zote zilizobaki na ametoa nafasi kwa daktari kuendelea na uchunguzi.

Man United inaendelea kuwatumia mabeki wa kati Chris Smalling, Phil Jones au Victor Linderlof aliyesajiliwa na klabu hiyo majira ya kiangazi msimu uliopita.
 
Mechi ya watani wa jadi mjini Belgrad kati ya Red Star na Partizan imeisha kwa mkong’oto uwanjani baada ya mashabiki wa Partizan wenyewe kutofautiana kauli.

Mashabiki 17 wamejuruhiwa kutokana na ugomvi uliozuka uwanjani hapo, huku baada yao wakiwahishwa hosptitali kutokana na kuumia zaidi.

Timbwili hilo lilitokea kabla ya dakika 10 mchezo kumalizika, ambapo wachezaji wa Partizan timu moja walitofautiana wenyewe kwa wenyewe wakati wakiendelea kushangilia.

Hata hivyo, habari zilieleza kwamba chanzo cha ugomvi huo ni kutokana na matatizo ya ujinga wao wenyewe kwani wangeweza kumaliza tofauti zao.
 
Real Madrid imeitungua mabao 2-1 klabu ya Al Jazira na bao la Greth Bale lilitosha kuipeleka timu yake kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa vilabu.

Bahati ya mtende ilikuwa kwa Bale, baada ya kugusa mpira mara ya kwanza na hakufanya makosa kutokana ana kuiandikia Madrid bao la ushindi dakika ya 81.

Awali, Cristiano Ronaldo aliisawazishia timu yake bao dakika ya 53 ikiwa ni siku chache zimepita tangu aliposherehekea tuzo yake ya Ballon d’Or kwa mara ya tano.
 
5434295df9d037a191cfc1d076164135.jpg
 
Back
Top Bottom