Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bila shaka, usingizi ni muhimu kwa afya ya mwili na ya akili. Kulingana na mtafiti William Dement, mwanzilishi wa kituo cha kwanza cha kuchunguza usingizi katika Chuo Kikuu cha Stanford Marekani, “inaonekana kiwango cha usingizi ambacho mtu hulala ndilo jambo muhimu zaidi ambalo huamua muda atakaoishi
 
Deborah Suchecki, mtafiti kwenye kituo cha kuchunguza usingizi huko São Paulo, Brazili, anasema hivi: “Kama watu wangalijua jinsi kutolala usingizi kunavyoathiri mwili, hawangalisema kwamba kulala ni kupoteza wakati au ni uvivu.”.
 
IMG_2949.jpg

Nawatakia Ijumaa njema wandugu!
 
AINA TATU ZA UFUNGAJI WA NDOA KISHERIA.

Sheria ya ndoa inatambua aina 3 za ufungaji wa ndoa yaani kiserikali, kidini na kimila.
Ndoa hizo zaweza kufungwa kwa kufuata taratibu za kidini au za kiserikali. Utaratibu huo utafuata au kuzingatia kama wanandoa ni waumini wa dhehebu Fulani au la.
 
(a) NDOA YA KIDINI:
Ndoa hii hufungwa kwa mujibu wa taratibu ya dini husika. Ni lazima masharti yote yatimizwe kisheria na taarifa ya nia ya kufunga ndoa itolewe na ndoa ifungiwe mahali pa wazi panapokubalika kisheria na mfungishaji awe na mamlaka hayo kisheria.
 
(b) NDOA YA KISERIKALI:
Ndoa hii hufungwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ambaye ndiye Msajili wa Ndoa. Ndoa itafungiwa katika ofisi ya Msajili au mahali pengine popote palipotajwa katika leseni yake ya kufungisha ndoa.
 
Back
Top Bottom