Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20171216-WA0003.jpg
 
Kutokana na mlolongo wa matokeo yasiyoridhisha tangu walipofungwa na Man United kwenye uwanja wao, bosi wa Arsenal amefunguka kuwa kipigo kinawatesa
Bosi wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa timu yake bado inahaha kuzoea kipigo cha nyumbani dhidi ya Manchester United mapema mwezi huu.
Gunners walitawala mchezo wote na kufanya mabadiliko bora katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Uingereza mnamo Desemba 2, lakini kipa wa upande wa pili David de Gea alikuwa na kiwango safi Arsenal waliponyukwa 3-1.
Klabu hiyo ya London imepata sare dhidi ya Southampton na West Ham United tangu mechi ya United, na Wenger amekiri kuwa kipigo hicho bado kimo kwenye akili za wachezaji wake.
"Bado kinazunguka akilini mwetu.Tunahitaji kuondoa hiyo. Ukiwa na nafasi nyingi kama tulizokuwa nazo na unatoka bila kitu, ni vigumu kukubaliana na hali halisi na itatuchukua muda kuzoea," Wenger aliwaambia waandishi.
"Nadhani njia bora ni kuendelea kusahau hilo na kuelekeza akilikwenye ubora wa mechi zetu."
Arsenal wamedondoka hadi nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza, na watakuwa wakitaka kupanda tena juu watakapoikabili Newcastle United Jumamosi mchana.
 
Back
Top Bottom