Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Kocha wa Real Madrid ameshindwa kukanusha au kukubali kama timu yao ina mpango wa kumsajili Mohamed Salah, lakini amekiri kumhusudu mchezaji huyo
Bosi wa Real Madrid Zinedine Zidane amemtaja Mohamed Salah kuwa "mchezaji mahiri" kufuatia madai kuwa mabingwa wa Hispania na Ulaa wanavutiwa na saini ya mshambuliaji huyo.
Salah alifunga mara 19 na kutoa pasi sita za goli katika mechi 25 za michuano yote kwenye klabu hiyo ya Uingereza msimu huu.
Mmisri huyo mwenye umri wa miaka 25 aliiwezesha nchi yake kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1990, na amehusishwa na tetesi za kutaka kutua Real Madrid wiki za hivi karibuni.
Mapema mwezi huu meneja wa Misri Hector Cuper alidai kuwa Los Blancos wanavutiwa kumsajili Salah.
Zidane alikataa kuthibitisha au kukanusha kama timu yake itafanya mchakato wa kumsajili mshambuliaji huyo, lakini Mfaransa huyo amemwagia sifa tele mchezaji huyo aliyesaini miaka mitano Liverpool akitokea Roma majira ya joto.
"Ni mchezaji mahiri. Kwanza akiwa Roma na sasa Liverpool, Ni mwanasoka muhimu na anakua siku kwa siku, ni mdogo na ninamkubali sana," Zidane aliwaambia waandishi.
Real Madrid wanatafuta ubingwa wa tatu Kombe la Dunia la Klabu watakapoikabili Gremio ya Brazili fainali ya Jumamosi.