Kuna hatari Taifa letu la Tanzania kugeuka kuwa jalala na hodi za waathirika wa dawa za kulevya, tusipokubari kufanya maamuzi ya busara katika kuishauri jamii kuacha na kuepuka kutumia dawa za kulevya.
kuna aina mbali mbali za dawa za kulevya zenye athari nyingi na kubwa katika miili yetu,maisha yetu na hata vizazi vijavyo iwapo tukiendelea kuto wasaidia waathirika wa dawa hizo za kulevya. Kwa mfano kuwapa ushauri kuweza kufika katika zahanati zilizokaribu ili kuanza tiba mapema.
Sii mimi peke yangu ambaye ninashuhudia waathirika wengi wa dawa za kulevya wanavyo pata tabu bali kila mtu anajionea kinachoendelea katika Taifa letu.Waathirika wengi hutengwa na ndugu na jamaa, marafiki na hata majirani, baada yakuwa wamekwisha poteza mwelekeo wa utimamu.
Isipokuwa mwanzo huwezi kutambua kuwa unaathirika au la.Kuna dawa nyingine huchukuwa muda mrefu kuonyesha dalili, ila unashauriwa kujitambua kiafya mara kwa mara kwa kufanya vipimo vya mwili wako katika hospitali iliyoko karibu na wewe.
Bangi ni mmea ulio na asilimia kubwa ya watumiaji kulingana na takwimu za afya zinavyo onyesha.Mmea huu una rangi ya kijani ambao hutoa majani, maua na mbegu ambazo hutumika kama kilevi. Bangi hustawi karibu maeneo yote hapa nchini na hutumika zaidi kuliko dawa nyingine za kulevya.
Kulingana na matukio, takwimu za afya zinaonyesha kuwa bangi hupatikana kwa wingi katika mikoa ya Mara, Iringa, Arusha, Kilimanjaro, Shinyanga, Tabora, Kagera na Mbeya.
Mvutaji wa bangi hubakiza moshi mwingi kwenye mapafu kwa muda mrefu,moshi wa bangi unapoingia kwenye mapafu hutengeneza kitu kama lami ambayo huganda na kuathiri utendaji kazi wa mapafu.
Bangi husababisha madhara mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuumwa koo, kupata kikohozi na saratani ya mapafu, kuathirika kwa mfumo wa uzazi ikiwa ni pamoja na kuzaa watoto wenye mtindio wa ubongo na mabadiliko ya hedhi kwa wanawake.
Bangi pia hupoteza kumbu kumbu, kuchanganyikiwa, ukatili, ukorofi, uhalifu na kadharika. Pia kuna aina nyingi za sura tofauti za bangi kwa mfano, kuna mafuta ya bangi, bangi kavu na bangi iliyo sindikwa.
Heroin ni aina ya dawa ya kulevya itokanayo na mmea unaojulikana kama “Opium poppy”dawa hii hupumbaza mfumo wa fahamu.
Kwamujiu wa ripoti za taasisi za afya zinaonyesha kuwa Heroin huingizwa nchini ikitokea nchi za mashariki ya mbali kama Afghanistani, Pakistan, Thailand, India n.k.
Mirungi ni aina ya mimea inayostawi kwenye hali ya unyevu nyevu na milima yenye urefu kati ya futi 4000 hadi 9000. Hapa nchini mimea hii hupatikana kwa wingi kama uoto wa asili katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro,Manyara na Tanga, hata hivo kulingana na uchunguzi mirngi mingi itumikayo nchini kwa kiasi kikubwa hutoka nchini Kenya.
Matumizi:
Heroin hutumika kwa kuvuta, kunusa unga, kunusa moshi na kujidunga sindano.Kuna madhara mengi sana yatokanayo na utumiaji wa dawa hii aina ya “heroin” ambayo asilimia 100 hutoka katika nchi za ughaibuni, madhara hayo hujitokeza katika mengi kama, mtumiaji mwenye ujauzito na madhara ya kijamii kawa ujumla.
Mdhara hayo ni pamoja na kuharibika kwa mfumo wa ubongo na fahamu, mabadiliko ya hedhi kwa wanawake, kushuka kawa mapigo ya moyo, kupata kizungu zungu, kichefu chefu na kutapika, dozi kuwa husababisha kifo, mchanganyiko wa heroin na pombe huleta madhara makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na kifo cha ghafla.
Utumiaji wa heroin kwa njia ya kujidunga sindano husababisha maambukizi ya “Virusi vya Ukimwi” (VVU) na magonjwa mengine ya damu kutokana na kushirikiana sindano na vifaa vingine.
Madhara mengine ni kwa watumiaji wenye ujauzito, ambayo ni kupata matatizo ya moyo, upungufu wa damu, mamba kuharibika, kuzaliwa watoto njiti, watoto kupata matatizo ya kiafya ikiwemo kuchelewa kukuwa kiakili na kimwili pia kujifungua watoo ambao mara nyingi hufa wakiwa chini ya umri wa miaka mitano.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.