Japo uvutaji wa tumbaku una madhara mabaya sana kwa afya ya mvutaji, haina athari za mihemuko au kubadilisha tabia ya mtumiaji ukilinganishwa na utumiaji vibaya wa vileo vingine vya kawaida.
Kwa hivyo, siyo kileo cha msingi cha kushughulika na mshauri nasaha wa madawa. Mara kwa mara, unaweza kuwa na fursa ya kuwaeleza ama wanafunzi kuhusu madhara ya tumbaku.
Uvutaji wa tumbaku una uraibu mkubwa. katika nchi zilizostawi kiviwanda, ni muuaji namba moja na unaendelea kutishia afya ya binadamu ulimwenguni kota.
Hii ndiyo bidhaa ya pekee inayopatikana kihalali kote duniani ambayo hudhuru afya ya binadamu ikitumiwa ilivyokusudiwa. Aidha, inajulikana kwa kusabibisha vifo vingi kuliko vileo vyote vinavyoamsha akili.
Ni tatizo la afya muhimu sana linalozuilika katika nchi zilizoendelea. kama tukiendelea na mtindo huu wa sasa, vifo kutokana na tumbaku duniani kote vinatarajiwa kufikia milioni kumi kila mwaka au zaidi ya asilimia kumi ya vifo vyote duniani itimiapo robo ya pili ya karne hii.
Utumiaji wa tumbaku na wanawake wajawazito waweza kuzua matatizo yanayohusiana na mimba, kupunguza ukuaji wa mimba yenyewe, uzani mwepesi wakati wa kuzaliwa, kuzaliwa kwa watoto kabla ya kufikisha muda wao, kuharibika kwa mimba,
watoto kuzaliwa wakiwa wafu, watoto kufa wazaliwapo na vifo vya watoto wachanga. matokeo ya kudumu kwa mtoto mchanga ni kama kudumuza ukuaji wa mwili na akili wa mtoto.
Ushahidi wa hivi majuzi pia ulithibitisha kuwa uvutaji hudhoofisha kinga mwilini na hivyo kutia hatarini zaidi kinga ya wavutaji tumbaku wenye virusi vya UKIMWI.
Ushahidi wa hivi majuzi pia ulithibitisha kuwa uvutaji hudhoofisha kinga mwilini na hivyo kutia hatarini zaidi kinga ya wavutaji tumbaku wenye virusi vya UKIMWI.
Kwa sasa uvutaji tumbaku unasababisha asilimia tisini ya saratani ya mapafu, ambayo ni asilimia thelathini ya saratani zote zikiwekwa pamoja. Zaidi ya asilimia themanini ya ugonjwa sugu wa kifua pamoja na asilimia ishirini hadi ishirini na tano ya magonjwa yote ya moyo na kupooza husababishwa na uvutaji tumbaku.
Wasiovuta kama vile watoto, wanapovuta moshi wa sigara katika chumba kisichoingiza hewa safi wakiwa na mvutaji huweza kupatawa na magonjwa ya matatizo ya kupumua, hasa kwa watoto.
Kokein
Mmea wa koka (trythroxylon coca) ni gugu lisilokauka lipatikanalo kwa wingi katika maeneo ya Marekani kusini mwa Mlima wa Andes. Kiungo chake tendaji ni alkaloid cokeini, uvumbi mweupe utolewao katika majani yake kwa njia urahisi. Kokeini ni dawa yenye matokeo ya uchachawishi.
Utumiaji wa koka ulikuwa mazoea ya jadi katika baadhi ya maeneo ya tamaduni za kihindi katika Milima ya Andes. Hutumika kama chachawishi, ikiongeza nguvu stahimilivu za mwili na akili huku ikimaliza hamu ya kula na kunywa.
Utafunaji wa matawi ya koka ulijulikana pia kuwa una sehemu muhimu katika shughuli za mila na sherehe za baadhi ya makabila asili ya Marekani kusini, ikichachawisha ukariri wa mkusanyo wa visasili na ufufuaji wa kumbukumbu za kihistoria kupitia usimulizi wa hadithi.
Ukuzaji haramu wa kokeini duniani umeongezeka maradufu kati ya miaka 1985 na 1994. Jambo hili limesababisha ongezeko la biashara ya mihadarati na hivyo kueneza dawa hiyo katika maeneo mapya ya kijiografia hata kufikia sehemu za Afrika.
Uvumbi wa kokeini hutumizwa kwa njia ya kunisisha puani. Aidha, uvumbi waweza kupashwa na kugandishwa kuwa dutu ngumu yanye nguvu zaidi iitwayo kokeini 'ceack', ambayo yaweza kuvutwa kwenye kiko au kuyeyushwa majini na kudungwa kwa sindano.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.