Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hata hivyo, anasisitiza kuwa tatizo hili linaweza kwisha kama litakuwa katika hatua za awali. Kwa wenye tatizo lililokomaa watalazimika kufuata matibabu kulingana na ukubwa wake.
 
Haja kubwa huganda katika kuta za utumbo, hali hii huifanya haja izunguke kwa muda mrefu na ndiyo tatizo hili huanzia hapa,” anasema na kuongeza:
“Unapojisaidia ukiwa umekaa, ile njia ya haja kubwa huwa kama imejifunga, inabidi utumie nguvu nyingi sasa ukiwa na tatizo hili la kukosa haja kubwa huifanya itoke kwa uchache zaidi,” anasema Dk Sikirov
 
Aidha, anasema kupata haja kubwa mara kwa mara ni muhimu kwa kuwa usipoitoa maana yake inazungusha sumu katika damu jambo ambalo ni hatari kwa afya.
Anaongeza kuwa kutopata haja kubwa ni kichocheo chenye uwezo mkubwa wa kusababisha saratani ya utumbo mkubwa na uambukizi katika kidole tumbo.
 
Tafsiri ya kitabibu inasema hali ya kukosa haja kubwa ni pale mtu anaposhindwa kuipata angalau mara tatu kwa wiki. Hata hivyo, ili ujue afya yako ni njema unapaswa kuwa unapata haja kubwa angalau mara moja kila siku.
 
Daktari Denis Burkitt aliwahi kuandika kitabu cha maelekezo ya chakula ili kuepuka ugonjwa wa saratani. Katika kitabu hicho alieleza namna ambavyo watu wanaweza kujikinga na saratani za aina mbalimbali.
 
Akizungumzia saratani ya utumbo mpana pamoja na kuelezea vyakula na aina ya maisha, pia aliwaasa watu kutumia choo cha kukaa ili kujiepusha na tatizo hilo.
Anaeleza kuwa kwa Marekani pekee, watu zaidi ya 150,000 hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa saratani ya utumbo mkubwa.
 
Mtaalamu wa Ngozi katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba Muhimbili (MUHAS), Profesa Kisali Pallangyo anasema matumizi ya vyoo hivyo yanaweza kuwa chanzo cha maambukizi ya magonjwa ya ngozi. Profesa Pallangyo anasema ni rahisi kuambukizwa magonjwa ya ngono na ngozi kwa urahisi pale unapotumia vyoo vya kukaa tofauti na vile vya kuchuchumaa.
 
Mtu mwenye magonjwa ya ngozi au ya ngono, anaweza kuyaacha katika ‘sink’ anapolikalia, hivyo ni rahisi kwa mtu mwingine ‘kuyachukua’ mara atakapokaa wakati wa kujisaidia,” anasema Prof Pallangyo.
 
Kweli..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…