Achari hii kuwatia moyo wale wengine waliokuwa hawana uwezo wa kununua samaki kila siku.
Kuwafanya awe na hamu ya kutengenza achari kama hii kwani kutengenza achari kama hii ni nzuri sana.
Achari ya mbirimbi
Mbirimbi ni kiungo kinachotokana na mti wa mbirimbi. Mti huu ambao unaasili ya kizanzbar ni maarufu sana hapa Zanzibar. Mbirimbi hutumika pamoja na mambo mengine kwa kutengenezea achari.
Mahitaji
Achari ya mbirimbi, unachukwa mbirimbi zako , na kuzitia kwenye chombo chako pamoja na maji , kisu , kibati , chumvi, bizari, kiutungu maji , pilipili , kuna baadhi ya watu hupasuwa nyemba nyemba , wengine kuzichuna kwa kibati.
Hifadhi
Uikmaliza hapo unazitia kwenye chupa yako iliyo safi pamoja na nakuchanganya chumvi, kitungu , bizari na kuzichanga pamoja na uweka sehemu ya jua na kuanika na kuchukwa muda kidogo mpaka zibadilike rangi yake ya kijani iliyokuwa nayo.
Hii inaweza kuchukuwa kati ya siku 7 mpaka wiki mbili kutegemea na kutoka kwa jua. Kumbuka kwamba kuanika achari ya mbirimbi ni lazima uli kuziepusha na kuoza ama kupata ukungu ambao kimsingi ni hatari kwa afya. Inapofikia kwenye kuelekea manjano ya kuvutia hapo inakuwa tayari kwa kuliwa.

Matumizi
Kwa kawaida achari ya mbirimbi…. Hutumika kama kiungo kwa ajili ya kuongeza uchachu katika mchuzi lakini pia inaweza kutumiwa moja kwa moja kwa kula na chakula kama wali wa kuchemsaha , sheli sheli na ndizi za kuchemsha.