Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Baada ya Tanzania kupitia kwa Kinana, Bunge la pili la Afrika la Mashariki liliongozwa na Spika Abdirahim Abdi kutoka Kenya. EALA ya tatu iliongozwa na Waganda wawili ndani ya miaka mitano, Margaret Zziwa na Dan Kidega. Swali linaulizwa ni kwa nini Tanzania isingewaachia Burundi na Rwanda wagombee?
 
Martin Ngoga wa Rwanda ameshachaguliwa wa Spika wa Bunge, lakini anapingwa na Burundi na Tanzania ambao wametishia kufungua kesi Mahakama ya Afrika Mashariki kwa madai kuwa Spika alichaguliwa bila akidi (quorum) kutimia, kwani wabunge wa Tanzania na Burundi hawakupo kushiriki uchaguzi.
 
Miezi mitatu shughuli za Bunge la Afrika Mashariki hazifanyiki, vikao vingi vilishaahirishwa kwa sababu ya kutokidhi akidi. Uchaguzi uliompitisha Ngoga haukidhi akidi, lakini inadaiwa wabunge wa Kenya na Uganda walimshurutisha Katibu wa Bunge, Kenneth Madete kufanya uchaguzi hivyohivyo.
 
Burundi wamewasilisha jina la Leontine Nzeimana na Tanzania ni Adam Kimbisa. Wabunge wa Uganda na Kenya wanalalamika kuwa kuna wakuu wa nchi za Afrika Mashariki wanataka kupanga kiongozi wa Bunge kitu ambacho si sawa.
 
Vyuma vina kutu

Wakati Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Rais Joseph Kabila anaendelea kurefusha muda wake wa kukaa madarakani na kusababisha mgogoro, Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza yupo kwenye mikakati ya kuusafishia njia utawala wake.
 
Uganda tayari Rais Yoweri Museveni ameshinda mapambano ya kubaki madarakani kwa miaka mingi ijayo baada ya Bunge kufuta kipengele cha ukomo wa umri wa mgombea urais, vilevile Bunge la Uganda limerefusha kipindi cha muhula wa uongozi kutoka miaka mitano mpaka saba.
 
Novemba mwaka huu, aliyekuwa Meya wa Caracas, Venezuela, Antonio Ledezma, alitoroka kizuizi za nyumbani (house arrest) na kutimkia Madrid, Hispania kisha Miami, Marekani. Kabla ya kuwekwa kizuizini, Ledzema alipata kuwekwa kwenye gereza la kijeshi tangu mwaka 2015.
 
Hakuna kosa ambalo Ledzema anafanya, isipokuwa ni yeye kuwa mpinzani. Halmashauri ya Jiji la Caracas ilifutwa na Rais wa Venezuela, Nicholas Maduro kwa sababu ilikuwa ikiongozwa na upinzani. Wanasiasa wa vyama vya upinzani Venezuela wana maisha magumu mno.
 
Septemba, wapinzani wengi nchini Rwanda walikamatwa, akiwamo Diane Rwigara ambaye anashikiliwa mpaka sasa akiwa na mama yake pamoja na dada yake. Watu wa haki za binadam wanapaza sauti kutaka wapinzani wa Rais Paul Kagame wasikamatwe isivyo haki lakini Diane, mama na dada yake hawajaachiwa.
 
Naam, vyuma vimekaza mpaka kupata kutu. Wapinzani Tanzania wamesusia uchaguzi mdogo wa marudio majimbo ya Singida Kaskazini, Songea Mjini na Longido wakidai kuwa kwa mchezo mbaya wa CCM uliofanywa kwenye uchaguzi wa madiwani kata 43 hivi karibuni, kisha Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kufumbia macho, kushiriki tena ni kutwanga maji kwenye kinu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…