Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa Israel kauli ya Trump ni ushindi mkubwa, maana miaka yote imekuwa ikiutambulisha Jerusalem kama mji mkuu wao lakini jumuiya za kimataifa hazikubaliani na hilo kwa sababu Mashariki ya Jerusalem inamilikiwa na Wapalestina. Unawaondoaje wakati ni mji wao wa kihistoria na kiimani?
 
Jerusalem hauishii kugombewa tu na Wapalestina na Waisrael kwa umiliki wa makazi, bali mji huo ni mtakatifu kwa imani za Kiislam, Kikristo na Kiyahudi. Hivyo, kauli yenye kuukabidhi mji wa Jerusalem kwa Israel peke ina hatari kubwa. Siyo tu kwa Palestina na Israel bali dunia nzima.
 
Nchi ambazo zinaunga mkono juhudi za Palestina kama dola huru tayari zimeshatoa kauli ya kuchukizwa na msimamo wa Marekani kuhusu Jerusalem. Tanzania imesisitiza ubalozi wake Israel utabaki Tel Aviv, chama tawala Afrika Kusini, ANC, kimeiagiza Serikali kuupunguzia hadhi ubalozi wake wa Israel.
 
Wakati nchi nyingi zikitoa hisia zake kuhusiana na msimamo wa Marekani juu ya Jerusalem, Trump amesema atakata misaada ya kifedha kwa nchi ambazo zitapinga uamuzi wake huo wa kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel. Hicho ni kipimo kuwa vyuma vimekaza kwelikweli.
 
Suala la mgogoro wa Israel na Palestina linalazimishwa. Si ajabu nchi nyingi ambazo zilikuwa kumbatio la Wapalestina, zikaanza kubadilika kwa hofu ya kukosa misaada. Trump anataka kutumia fedha kama kigezo cha kuzifanya nchi zinazoendelea kutii sera zake kwa lazima.
 
Dunia imejaa migogoro. Kila upande kuna mitifuano ya kisiasa. Kwingine viongozi wanalizwa na uamuzi wa wananchi wao, ila maeneo mengi wananchi wanateswa na viongozi wakandamizaji na wasiotii uhuru wa raia na demokrasia.
 
Hakuna wa kuvilegeza

Machi 29, Uingereza iliijulisha Jumuiya ya Ulaya (EU) juu ya kujitoa kwenye umoja huo ifikapo Machi 29, 2019. Uamuzi huo ulitokana na Waingereza kupiga kura Juni 23, 2016 na kwa wingi wao walichagua nchi yao kuondoka EU.
 
Kuondoka kwa Cameron ndipo kuingia kwa Theresa May. Hata hivyo, mazingira ya kibiashara ya Uingereza yanatajwa kuwa yatakuwa magumu kati yake na nchi wanachama wa EU, huku mpepesuko wa kiuchumi ukitabiriwa kulikumba Taifa hilo kuanzia Machi 29, 2019, itakapojiondoa rasmi.
 
Baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu Kenya Agosti 8, mwaka huu, maseneta na magavana wa majimbo ya Pwani, walifanya mkutano wa pamoja na kueleza dhamira yao ya kuanzisha mchakato wa kujitenga ili eneo la Pwani Kenya liwe nchi huru inayojitegemea.
 
Tangazo la mchakato huo wa majimbo ya Pwani Kenya kujitenga lilitoka kabla ya Mahakama ya Juu nchini Kenya haijatoa uamuzi wa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8 yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenya. Ilikuwa pia kabla ya uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26, mwaka huu na Uhuru kushinda tena kisha kuapishwa Novemba 28.
 
Desemba 21, Catalonia ilifanya uchaguzi wa wabunge, watakaounda Bunge la 12, baada ya uongozi mzima wa jimbo hilo kuondolewa ofisini na Waziri Mkuu wa Hispania, Mariano Rajoy, kwa kile alichosema kuwa viongozi waliokuwapo Catalonia walivunja ibara ya 155 ya Katiba ya Hispania ya mwaka 1978.
 
Oktoba 27, Catalonia ilifikia uamuzi mkubwa na wa kihistoria, baada ya Bunge lililovunjwa kupitisha maazimio ya jimbo hilo kujitenga na Hispania ili litambulike kama nchi huru na Jamhuri ya Catalonia. Uamuzi huo ulikuja baada ya harakati zilizoanza takriban miaka 100 iliyopita, kutaka isiwe sehemu ya Hispania.
 
Back
Top Bottom