Hapo zamani, kabla ya uvumbuzi wa insulin (1921), ugonjwa wa kisukari, Type 1 Diabetes, ulikuwa ni ugonjwa ulioua watu wengi sana miaka michache tu baada ya mtu kuupata ugonjwa huo.
Lakini sasa mambo yamebadilika kwa kiasi kikubwa sana. Mtu mwenye ugonjwa huu anaweza kuishi maisha ya kawaida kabisa, ili mradi anakuwa na mpango mzuri wa chakula, mazoezi ya kutosha na anatumia insulin.
Kuwa mgonjwa wa kisukari maana yake ni kubali namna ya kuishi na siyo kushindwa kufanya jambo lo lote lile ulilokusudia. Unaweza kufanya biashara zako, kushiriki michezo na kufikia malengo yako bila tatizo lo lote.
Kuna orodha ya watu wengi waliokuwa na kisukari na wakafanya vizuri katika michezo, siasa, uigizaji wa filamu, muziki, uandishi wa habari n.k. kinachotakiwa ni mpango wa kula, mazoezi ya kutosha na kuzingatia tiba unayopewa na daktari wako.
Hakuna sababu KAMWE ya kushindwa kufikia malengo yako. Mfano mzuri ni Sir Steven Redgrave, mwanamichezo aliyeweza kunyakua medali za dhahabu katika michezo ya Olympiki kwa miaka mitano mfululizo akiwa mwathirika wa Type 1 Diabetes kuanzia mwaka 1997.