Pia kuna nyaraka nilizozipelekaTakukuru zikionyesha wengine walioshiriki katika wizi wa fedha hizo, naomba niendelee kuwa hai ili niweze kutoa ushahidi mzuri kuhusu wezi wa fedha hizo.”
Mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh Sethi ameieleza Mahakama kuwa yuko tayari kutoa ushirikiano ikiwemo nyaraka zitakazoitajika.
Hata hivyo, wakili Swai alieleza Mahakama kuwa zipo nyaraka ambazo Rugemarila aliwasilisha ofisini na zinafanyiwa kazi kisha watatoa majibu baada ya kukamilika.
Hakimu Simba alisema afya za washtakiwa ni muhimu wanatakiwa kufanyiwa uchunguzi na kuutaka upande wa mashtaka ukamilishe upelelezi kwa wakati.
Kesi hiyo imeairishwa hadi Januari 19, 2018 itakapotajwa tena.