Familia ya mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru imesema inasubiri baba yao apewe taarifa za msiba ili wajue taratibu za mazishi za mkewe Pares Mwiru.
Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Januari 5, 2017 nyumbani kwa Kingunge, mtoto wake Tonii Ngombale amesema baba yao hadi sasa bado hajapewa taarifa ya kifo cha mkewe.