Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Msemaji wa APRC, Seedy Njie, wiki iliyopita, alishutumu uamuzi wa tume ya rais ya kusaka ukweli kutaka kuuza ng’ombe pamoja na mali nyingine za Jammehs, akisema kitendo hicho kitakuwa kinyume na mamlaka ya Tume ya Janneh na itakuwa sawa na “wizi”.
 
Kutokana na amri hiyo haramu na isiyo ya haki ya Tume ya Janneh kuweka hadharani mali na mifugo ya rais wa zamani Jammeh kuanzia Jumapili ya 31 Desemba hadi Jumatano ya Januari 3 kwa ajili ya mnada (ambao nimeelezea kuwa ni udanganyifu wakati wa mahojiano Ijumaa kupitia redio), nimekuwa nikikutana na maofisa na kueleza masikitiko yangu kuwa uuzaji usitishwe kwani uko nje ya mamlaka ya Tumen a ni kukiuka kifungu cha 200, 201, 202 na haki ya kumiliki mali,” aliliambia gazeti la The Gambian Standard.
 
Jammeh aliyeanguka katika uchaguzi wa Desemba 2016 aliondoka Gambia baada ya utawala wake wa miongo miwili kuhitimishwa Januari 2017 na kwa sasa anaishi Equatorial Guinea. Bado hajatoa maoni yoyote kuhusiana na hali inayoendelea nyumbani tangu alipoondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…