1. Kuchelewa Kufungua Biashara
Kuna baadhi ya wamiliki wa biashara wanachelewa kufungua biashara na unakuta mteja anahitajia kupata huduma mapema ukilinganisha na muda wako ambao unafungua biashara sababu hii inaweza ikampoteza mteja
au kumkera kama tabia yako wewe kila siku ni kuchelewa mteja anakusubiri katika eneo la biashara badala ya wewe kumsubiri mteja sababu inaweza ikapelekea kumkera au kumpoteza mteja wako.
2. Kufanya Biashara kwa Mazoea/ Kujisikia
Unapokuwa umeamua kufanya biashara basi fanya kila siku bila mazoea au kujisikia kuna wafanyabiashara wengine wanafanya biashara kwa kujisikia au kwa mazoea kwa mfano,
leo anaweza kufungua kesho kafunga sasa tabia kama hii inaweza kumsababishia mteja kupata kero na kukuhama kabisa ukiamua kufanya biashara fanya kila siku bila kukata tama bila kujali siku yaani siku Fulani kuna wateja na siku Fulani hakuna wateja hivyo basi unaamua kutofanya biashara kwa hiyo acha kufanya biashara kwa mazoea.
3. Kuacha Biashara peke yake
Kuna tabia ya wafanyabiashara wanaweza kufungua biashara yao na kuacha peke yake anazungukazunguka au kwenda sehemu kupiga stori huku akiacha biashara yake wazi mteja akija anapata shida ya kumtafuta mtoa huduma
unafikiri kama kuna sehemu nyingine ambapo mteja huyu anaenda na kumkuta mtoa huduma yuko katika eneo lake la biashara kila siku je ataweza kushawishika tena kurudi kwako? Kama sehemu nyingine anahudumiwa vizuri?
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.