Kwa mujibu wa ‘Havard Medical School’ utafiti umeonyesha kuwa kulala kwa muda wa chini ya saa tano kwa siku huongeza hatari ya mtu kufa kwa asilimia 15.
Mfumo mkuu wa neva
Unapolala unaupa ubongo wako muda mzuri wa kupumzika na kuifanya kaze yake kwa utulivu. Vilevile ubongo hutengeneza protini ambayo husaidia kuzihuisha seli zilizoharibika.
Unapokosa usingizi wa kutosha ina maana kuwa ubongo wako haupati muda mzuri wa kujituliza, hivyo utaathiri uwezo wako wa kujifunza mambo mapya na kuhifadhi kumbukumbu.
Mfumo wa upumuaji
Unapokosa usingizi wa kutosha, ulinzi wa mwili wako dhidi ya magonjwa hupungua, hivyo kujiweka katika hatari ya kupata madhara katika mfumo mzima wa upumuaji.
Mfumo wa mmeng’enyo
Kwa mujibu wa utafiti mdogo uliofanywa na Havard Medical School, ulibaini kuwa kuna muunganiko kati ya kukosa usingizi na kuongezeka kwa uzito wa mwili.
Mfumo wa Kinga ya mwili
Unapokuwa umelala, kinga yako ya mwili hutengeneza seli za kupambana na bakteria, virusi, maradhi yanayouingia mwili pamoja na magonjwa mbalimbali.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ‘Mayo Clinic’ umeonyesha kuwa mtu asipopata usingizi wa kutosha anakuwa katika hatari kubwa ya mwili wake kushindwa kupambana na bakteria hatari wanaoingia.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.