Safina Mziray (25) ameolewa hivi karibuni lakini tayari ameingiwa na hofu hii kwakuwa hajui kama ndoa yake itadumu. Anasema kwamba lolote linaweza kutokea na kusababisha aachike.
Woga wa kuwaacha watoto na mfanyakazi
Bila shaka wanawake wanahofia usalama wa mtoto wake mchanga anapobaki na msaidizi wa kazi za nyumbani baada ya kuisha kwa likizo ya uzazi. Wengi wanafikiria kuwa watoto wao watateswa na wafanyakazi hawa, pia wanaamini hakuna anayeweza kumjali mwanae kwa upendo zaidi yake.
Huu ndio muda ninaokuwa na wasiwasi kupita kiasi. Nikiwa naangalia video za baadhi ya wafanyakazi wa ndani wanavyowatesa watoto, naanza kufikiria na wa kwangu atakuwa anafanyiwa hivi hivi,” anasema Diana (30) mama wa watoto wawili.
Woga wa mume kutokuwa muaminifu
Wapenzi mara zote wanaogopa wenza wao kutokuwa waaminifu. Wanasema kuwa mnaweza kufunga ndoa takatifu Kanisani na kwa sherehe kubwa sana na bado mkaendeleza mahusiano ya nje ya ndoa, jambo linaloleta migogoro isiyoisha.
Wanawake mara zote wanapenda kuwa kwenye mahusiano yanayodumu muda mrefu, lakini kama mambo yakibadilika , mara zote wanajikuta wanalazimika kuvumilia maumivu makali sana.
Wanawake mara zote wanapenda kuwa kwenye mahusiano yanayodumu muda mrefu, lakini kama mambo yakibadilika , mara zote wanajikuta wanalazimika kuvumilia maumivu makali sana.
Fatuma Ramadhan (27) anasema kuwa tangu aachane na mpenzi wake, amekuwa anaishi kwa woga sana. Mpenzi wake huyo kisirisiri alioa mwanamke mwengine, na toka hapo imani yake kwa wanaume imepotea kabisa na hawezi kuanzishwa mahusiano mengine.
Nilipokuja kugundua kuwa mpenzi wangu alikuwa na mwanamke mwengine niliumia sana na nilikuwa na wasiwasi muda wote. Ilikuwa ngumu sana kulivumilia,” amesema na kuongeza kuwa “…tangu muda huo siamini mwanaume yeyote yule. Najua kwamba wanaume wote wanafanana tabia na nimeamua kuwa peke yangu.”
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.