misuli hii itachoka na hivyo kuacha kufanyakazi kwa usahihi. Hilo linapotokea unashindwa kuzuia tena mkojo wako sababu misuli imelegea na hivyo mkojo ukija unapita moja kwa moja.
Hivyo, epuka kuharibu misuli hiyo kwa kubana mkojo kwa vitu ambavyo sio vya msingi. Kila unapohisi mkojo nenda kakojoe kisha rudi, endelea na ulichokuwa unafanya.
Maumivu
Kwa kawaida unaposhikilia mkojo kwenye kibofu kwa muda mrefu, unapatwa na maumivu makali, lakini maumivu hayo hutokomea mara tu unapokwenda haja ndogo. Maumivu hayo yanaweza yakawa ni mfumo wako wa maisha kama hutachukua tahadhari mapema.
Waswahili husema kuwa, tabia hujenga mazoea, na hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa misuli ya mwili wako, ukizoea kubana mkojo kila mara, itakua ikiima kila mara.
Kutanuka kibofu
Basi tusema kwamba ukibana mkojo kwa muda mrefu, kibofu chako kinaweza kisipasuke kutokana na wingi wa mkojo lakini kikatanuka kuliko ukubwa wake unaotakiwa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.