Jenner alitumia sindano kuchukua majimaji yaliyokuwa ndani ya vimbe hizo na kisha kuyapakaza maji hayo kwenye ngozi ya mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 8 ambaye alikuwa mtu wake wa kwanza kumfanyia majaribio ya kinga aliyotengeneza
Ingawa mtoto huyu alipata homa mwanzoni, ugonjwa wake ulipona haraka sana. Mwanasayansi huyu alipomchoma sindano yenye virusi vya tetekuwanga baada ya kupewa kinga – mtoto huyo hakuugua kabisa.
Mnamo Machi 20 mwaka 1800, mgunduzi wa maswala ya teknolojia raia wa Italia aliyejulikana kwa jina la Alessandro Volta alitengeneza betri ya kwanza kutumika duniani. Kwa sasa kampuni hii ya kutengeneza betri mbalimbali ina miaka 217 toka kuanzishwa kwake.
Wakati anazindua beetri hii ya kwanza, Volta aliipa jina la “kifaa cha kubuni cha kutoa umeme” alipoamua kupingana na dhana iliyokuwa kipindi hicho kwamba ilikuwa ni lazima tishu ya mnyama itumike ili kuweza kutengeneza umeme.
Badala yake, alitumia vipande vya chuma na nguo chakavu zilizoloweshwa kwenye maji. Hivi vilitosha kupitisha umeme na ndio ukawa mwanzo wa betri ya kwanza duniani.
Muda mfupi baada ya mgunduzi wa kisayansi Alexander Graham Bell kutambulisha ugunduzi wake mpya wa simu, karani wa kijerumani, Emile Berliner aligundua kwamba transmita ya simu hiyo ilikuwa na uwezo mdogo sana.
Katika mabadiliko yaliyokuwa yanafanyika ili watu wanaosumbuliwa na macho wasivae miwani, vioo hivi vilivyotengenezwa katika karne ya 19 vilitengenezwa na kioo kitupu na ilikuwa ni lazima mtu avae kioo hiki kwenye jicho lote.
Viongozi wa kampuni ya Bell walifurahishwa na maboresho haya hivyo kumuajiri moja kwa moja kwenye maabara ya ubunifu wa kampuni hiyo.
Katika mabadiliko yaliyokuwa yanafanyika ili watu wanaosumbuliwa na macho wasivae miwani, vioo hivi vilivyotengenezwa katika karne ya 19 vilitengenezwa na kioo kitupu na ilikuwa ni lazima mtu avae kioo hiki kwenye jicho lote.
Mwanzo vilikuwa vinajulikana kama “scleral lenses,” wakimaanisha sehemu nyeupe ya jicho, na viligunduliwa na mtengenezaji wa vifaa bandia vya macho, F.A. Mueller.
Historia inaonesha kuwa ngazi za umeme zilianza kutumika muda mfupi kabla ya kuanza kwa karne ya 20 na mgunduzi alikuwa ni mkazi wa jijini New York nchini Marekani, Jesse Reno.
Ugunduzi huu ulikubalika mara moja kwa waliokuwa na viwanda na migodi ya madini ambao walikuwa sasa hawalazimiki tena kupanda ngazi kwa miguu wawapo viwandani au kwenye migodi hiyo.
Mtengenezaji wa redio hii alikuwa ni fundi mkazi wa jijini New York – Marekani, A. H. Grebe ambaye alijaribu toleo la kwanza la redio ya aina hii ambapo baadaye ilisababisha kuweka mfumo wa redio ndani ya gari kuanzia mwanzoni mwa mwaka 1920.
Kwa msaada wa Daktari Henry Heimlich, msanii wa uchekeshaji Paul Winchell alisajili ugunduzi wake wa kubuni mchoro wa kwanza wa moyo wa bandia kwa ajili ya binadamu mwaka 1961.