Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

2. Kansa ya utumbo mkubwa:

Nyama nyekundu ikiliwa inakaa masaa ishirini kwenye mfumo wa chakula wa binadamu tofauti na vyakula vingine. Utafiti unaonyesha limbikizo hilo linaambatana sana na hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya utumbo mkubwa. Lakini madhara ya haya yameonekana kutokuwepo kwa kula nyama nyeupe.
 
3. Ugonjwa wa kisukari:

Watu wanaokula nyama na wasiokula nyama baada ya kufuatiliwa kwa muda wa miaka kumi mfulululizo[cohort studies}… watu wanaokula nyama wameonekana kupata ugonjwa wa kisukari sana kuliko wale wasiokula.
 
4. Ugonjwa wa kifafa:

Minyoo inyopatikana kwenye nguruwe kitaalamu kama taenia solium hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya fahamu ya ubongo hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa nacho kabisa. Halii hii inaweza kuzuiliwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive.
 
5.Unene uliopitiliza:

Nyama nyekundu ina kiwango kikubwa cha mafuta ambacho watu wengi hula mafuta hayo kama yalivyo mfano kwenye nyama ya nguruwe.unene na kitambi ni hatari sana kwana husababisha matatizo mengi ya kiafya na kisaikolojia, vifo vya ghafla vikiwa hatari zaidi kwenye swala la unene.
 
Hitimishao:

Nyama tunazokula siku hizi sio nyama halisi tena ukiangaliwa nyama ya kuku inayoliwa sana kwenye miji mikubwa na hotel kubwa namaanisha kuku sa kisasa, zinakuzwa kwa kemikali nyingi sana ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu na hata ladha yake ni tofauti kabisa na kuku wa kienyeji. Lakini kwasababu wamiliki wa biashara za nyama ni watu wenye fedha nyingi sana duniani ukweli huu hufichwa.
 
Vyanzo vinavyoweza kusababisha mlipuko wowote wa uvimbe mwilini na magonjwa mengini ya aina hiyo ni vingi, kutokana na aina ya vyakula tunavyokula, mazingira tunayoishi na hata msongo wa mawazo unaosababishwa na kazi tunazozifanya.
 
Ili mwili uwe na uwezo huo, unahitaji uupe uwezo kwa kula vyakula vinavyoongeza kinga mwilini, hasa kinga ya kuzuia uvimbe, miongoni mwa hivyo ni pamoja na hivi vifuatavyo:
 
MAHARAGE
Jamii yote ya maharage, ikiwemo na soya, inaaminika kuwa na kiasi kingi cha protini na virutubisho vingine vingi vinavyohitajika mwilini kuzuia magonjwa ya mlipuko na uvimbe. Pia vyakula hivi vinafaa kwa wagonjwa wa moyo.
 
SAMAKI NA MAFUTA YAKE
Ulaji wa samaki, hasa aina ya jodari, ni muhimu sana, kwani samaki hawa wana kiwango kingi cha virutubisho aina Omega-3 na 6. Ukiweza, pendelea kula samaki kila mara katika mlo wako wa kila siku.
 
Miti hii ina kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya uvimbe. Hivyo hakikisha kwenye mapishi yako, unaangalia namna ya kuchanganya viungo hivi.
 
VIAZI VITAMU
Viazi vitamu vina kiwango kikubwa pia cha virutubisho vyenye uwezo wa kung’arisha ngozi, kuimarisha kinga ya mwili na pia afya ya moyo. Kwa upande wa kuzuia magonjwa ya uvimbe, viazi pia vimetajwa kuwa na uwezo mkubwa sana. Mbali ya viazi, pia hata maboga na karoti nazo zina virutubisho vingi vya kuimarisha kinga ya mwili.
 
CHAI
Unaweza kupamba na magonjwa ya uvimbe na kuupa mwili wako kinga ya mwili dhidi ya magonjwa hayo hata kwa kunywa chai, hasa ya majani ya kijani (green tea), ambayo utafiti wa kitabibu unaonesha kuwa na kiwango kingi cha virutubisho vya kuongeza kinga ya mwili.
 
Back
Top Bottom