Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unapaswa kutambua pia maneno unayoyasema au kuyaandika. Hii ina maana kwamba, kabla hujaandika au kusema jambo, uwe unajiuliza kwanza. Kila linalotoka mdomoni mwako au mkononi mwako(Kuandika) liwe limepata kibali chako baada ya kulitafakari na kuona halitasababisha madhara kwako au kwa wengine.
 
Usizungumze kwa sauti ya juu sana au ya chini sana wala usikubai kuchotwa na mtu anayefoka, nawe ukaanza kufoka. Wacha anayefoka afoke huku ukijua wazi kwamba, anajiumiza bure, huku wewe ukiwa huna haja ya kujiumiza. Kumbuka kwamba, kufoka ni kujitetea kwa sauti kuliko mantiki. Usikubali kuwa dhaifu wa kiwango hicho.
 
Jaribu kutafuta muda, tuseme wakati wa mapumziko la mchana. Tafuta mahali palipotulia, kaa hapo na kujaribu kupeleka mawazo yako kwenye eneo lenye mandhari inayopendeza.
 
Yapeleke hapo, yakae kwa muda wa kutosha. Kama siyo mandhari, basi kumbuka tukio lolote huko nyuma ambalo liliwahi kukufurahisha sana. Liweke mawazoni mwako kwa muda wa kutosha.
 
Jaribu kuweka mawazo yako yote kwenye kile unachokifanya kwa wakati huo. Hii itakuwezesha kutokuingiza mawazo yenye kukera kwenye mfumo wako wa kufikiri.
 
Badala ya kupoteza muda na nguvu kwa kujiuliza sababu za watu kufanya mambo fulani dhidi yako au kuhusu tabia usizozipenda kwa baadhi ya watu, ni botra kuweka nguvu na mawazo yako kwenye namna utakavyoweza kuboresha vitendo vyako.
 
Kabla hujazungumza na mtu anayekukera au unayemwogopa ama pengine usiyempenda, pumua polepole kwa kina, ukivuta pumzi ndani na kuzitoa nje, kiasi cha mara tatu na tengeneza picha kwenye mawazo yako, ukijiona kuwa mnazungumza kwa amani na upendo na mtu huyo.
 
d06b0fb73e87e1f17931ed37516f907c.jpg
 
Back
Top Bottom