Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

SULUHISHO
Kunywa maji ya kutosha kulingana na uzito wa kazi unazozifanya. Kiwango cha chini ni angalau lita moja ya maji safi na salama, hakikisha umekunywa maji hata kama husikii kiu.
 
Vile vile ulaji wa matunda na unywaji wa juisi zitokanazo na matunda au mboga mboga, huweza kuondoa upungufu wa maji mwilini.
 
KUKOSA HAJA KUBWA
Kitendo cha kukaa zaidi ya siku moja bila kupata haja kubwa ni dalili ya wazi ya ukosefu wa kamba lishe (fibre) mwilini. Kwa kawaida binadamu anatakiwa kupata choo kikubwa kila siku kilicho laini na kingi.
 
Iwapo hupati choo kila siku na ukipata unapata kigumu, tena kidogo, jua una matatizo!
Haja kubwa ni muhimu kwa sababu ndiyo inayosafisha tumbo, uchafu unapokaa tumboni kwa muda mrefu,
 
Iwapo hupati choo kila siku na ukipata unapata kigumu, tena kidogo, jua una matatizo!
Haja kubwa ni muhimu kwa sababu ndiyo inayosafisha tumbo, uchafu unapokaa tumboni kwa muda mrefu,
 
sumu zilizomo kwenye haja kubwa hurejea mwilini na husababisha matatizo mengi ya kiafya, kuanzia magonjwa ya uvimbe, moyo na hata ubongo. Sumu huvuruga pia mtiririko wa homoni mwilini na hudhoofisha kinga ya mwili.
 
SULUHISHO
Kula kwa wingi matunda mbalimbali, mboga za majani na vyakula vitokanavyo na nafaka zisizokobolewa, kama vile ugali wa dona, mtama, ulezi, n.k.
 
Ulaji wa vyakula hivyo bora, siyo tu kutaondoa tatizo la ukosefu wa haja kubwa, bali vitakulinda pia dhidi ya magonjwa ya kisukari, presha, ugonjwa wa moyo na mengine mengi.
 
VIDONDA PEMBENI MWA MDOMO
Utafiti umeonesha kwamba kupasuka kwa midomo na kutokea kwa vidonda pembeni ya midomo, huwa ni dalili moja wapo ya upungufu wa vitamini B mwilini na mara nyingi huwatokea watu wanaopenda kunywa kilevi kupita kiasi, kula vyakula vya kwenye makopo (processed foods) na kula sukari kwa wingi.
 
SULUHISHO
Suluhisho ni kula vyakula vyenye kuongeza vitamin B kwa wingi. Miongoni mwa vyakula vyenye kiwango kingi cha vitamin B ni pamoja na kiini cha mayai ya kienyeji, viazi vitamu, nyama ya ng’ombe na ya kuku, maini na vyakula vitokanavyo na nafaka isiyokobolewa.
 
Ingawa unaweza pia kula vidonge lishe vya vitamin B ili kuondoa upungufu huo, lakini tahadhari lazima ichukuliwe na ina shauriwa kula vyakula vya kuongeza vitamini hiyo zaidi kuliko vidonge.
 
Hatujaribu kumhukumu mtu yeyote kwa mazoea yake. Kila mmoja ana uhuru wa kutumia simu yake kufanya anachojisikia yeye (hata ikiwa ni kwa kuangalia video za ngono kutoka mtandaoni au zilizohifadhiwa ndani ya kifaa hicho).
 
Lakini inatakiwa uwe makini kama kuwa unapakua app za bure za ngono kwa kutumia simu yako ya Android, kama ambavyo mtaalamu wa ulinzi mtandaoni wa kampuni ya teknolojia ya Dell, Alex Dubrovsky alipogundua kwamba kuna udukuzi unaofanywa ili kuziathiri app hizo.
 
Wadukuzi wametengeneza mfumo wa kuiathiri simu unaofichwa ndani ya app hizo ambazo zina uwezo wa kuifunga simu ya mtumiaji na hata kukuzuia usiweze kuifuta app hiyo kutoka kwenye simu yako unapotaka kufanya hivyo.
 
Dubrovsky na timu yake ya watafiti walmebainisha kuwa wadukuzi wana uhakika kabisa wa kutumia app za ngono kufanya mashambulizi yao: mtumiaji anapakua app na kuwapa wadukuzi njia ya kuingia kwenye simu yako na kuitumia kama ipo kiganjani kwake na kwamba inawapa uwezo wa kufanya chochote. Na kwa wale wanatumia Android toleo la 4.4 KitKat, wadukuzi wanaweza kuifunga kabisa simu yako na kukuzuia usiweze kuifungua tena kama wakitaka.
 
Kutokana na teknolojia ya sasa, ushambuliaji wa aina hii bado unafanywa kwa kiwango kidogo lakini inaelekea utaongezeka kwa kasi kadri muda unavyosonga mbele,” ameandika Dubrovsky. “Kinachoshangaza ni kwamba mpaka sasa, waliofanyiwa udukuzi huu hawajawahi kuombwa pesa ili simu zao zifunguliwet, na pia kwakuwa bado waliokumbana na udukuzi huu wameweza kutumia tena simu zao ni ishara kwamba mfumo huu wa udukuzi haujaanza kutumiwa kwa kiwango cha juu.”
 
Kwahiyo, ingawa aina hii ya udukuzi bado ipo kwenye hatua za awali ambao kwa sasa walengwa ni watumiaji wa mifumo ya zamani ya simu za Android na kwa kutumia app za ngono pekee, inatabiriwa kuwa baada ya muda udukuzi huu utatumiwa kwenye mifumo ya kisasa zaidi na app nyingine nyingi zaidi (kama wadukuzi wakiweza kupita kwenye mfumo wa ulinzi wa Google).
 
Mapengo yanasababisha madhara makubwa kiafya zaidi ya lile wanaloliona wengi la kupunguza uzuri wa muonekano wa mtu. Hata hivyo, kama utamuona daktari wako katika muda sahihi na kujadiliana la kufanya kuhusu pengo/mapengo yako na kuyaziba na kupata tiba sahihi, unaweza kutunza afya ya kinywa chako kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu sana.
 
Baadhi ya tiba zilizozoeleka kwenye kuziba mapengo ni kuweka meno ya bandia yanayotoka, kuweka meno ya bandia ya kudumu au kupandikiza meno mengine ili kuziba pengo/mapengo yaliyopo.
 
Wakati mwingine, mgonjwa hushauriwa kutumia njia mbili kwa wakati mmoja, kuweka meno ya bandia yanayotoka na kuweka yale ya bandia ya kudumu. Yafuatayo ni baadhi ya madhara ya afya ya kinywa yanayoweza kusababishwa na mapengo.
 
Back
Top Bottom