Wanafunzi wanaosoma taaluma mbalimbali katika ngazi ya PhD huwa na muda mwingi katika masomo, ambao huutumia kufanya tafiti za masomo ili kuthibitisha kama unastahili kutunikiwa Shahada ya Udaktari (PhD).
Wanafunzi wa PhD. hukumbwa na vikwazo mbalimbali katika kipindi cha masomo kama msongo wa mawazo kutokana kutochapishwa kwa tafiti zao, pia tabia ya unyanyasaji au ukosefu wasimamizi ambao hawana uzoefu wa kutosha. Utafiti uliochapishwa katika jarida la Research Policy nchini Uingereza mwaka huu,
unasema kuwa msongo wa mawazo unaweza kuwa na athari kwa akili ya wanafunzi wa PhD. Takribani theluthi moja (1/3) ya wanafunzi wanaosoma PhD. wapo katika hatari ya kupata matatizo ya akili.
Uchunguzi ulifanywa kwa wanafunzi 3,659 kutoka vyuo vikuu huko Flanders, Ubelgiji, kwa wanafunzi wa masomo ya Sayansi au Humanities. Hata hivyo, matokeo ya uchunguzi huo yalionesha jinsi taaluma inavyoathiri afya ya akili.
Asilimia 51 ya watu waliofanyiwa utafiti walingundulika kuwa na dalili aina mbili za matatizo ya akili, huku asilimia 32 waliripotiwa kuwa na dalili aina nne. Kiwango hicho kilikuwa cha juu mara mbili zaidi ya idadi ya watu wenye elimu ya juu.
Baadhi ya dalili za kawaida ambazo wanafunzi waliripoti kuwa nazo ni pamoja kupoteza usingizi kutokana na hofu au wasiwasi na kutoweza kufurahia shughuli zao za kila siku. Watafiti pia waligundua kuwa jambo kubwa linalosababisha matatizo ya akili ilikuwa ni kushindwa kutimiza mahitaji ya familia kutokana na kazi nyingi, uhitaji mkubwa wa masomo ya PhD na kushindwa kudhibiti kazi wanazopewa.
Mwanafunzi wa PhD kutoka chuo cha Imperial nchini Uingereza, Claire anasema kusoma katika ngazi ya Uzamivu kuna uwezekano wa kuathiri afya ya akili ya mtu. Anasema baadhi ya marafiki zake walifikiria kuacha kuendelea na chuo katikati ya masomo yao.
Claire anaelezea kuwa alianza kusikia maumivu ya mwili, mafua makali na homa. Hata hivyo, vipimo vya damu vilionesha kuwa hakuna tatizo lolote, ingawa madaktari walimwambia hali kama hiyo inawezekana inahusiana na msongo wa mawazo.
Hata hivyo, anasema kuwa si kila mtu anayesomea PhD anaelewana na msimamizi wake, ukweli ni kwamba, baadhi ya wasimamizi hawana msaada na manufaa, bali hudharau wanafunzi.
Ripoti ya Research Policy inasema mfumo wa wasimamizi kwa wanafunzi wa PhD ulionekana ni jambo linalochangia matatizo ya akili kwa wanafunzi. Research Policy wanapendekeza kuwa vyuo vikuu viongeze juhudi zao katika kufuatilia wanafunzi wenye matatizo akili na kuongeza mbinu za usimamizi na kutambua kwa ujumla hatari na sababu za msingi.
Naye Nathan Vanderford, mwalimu msaidizi katika Chuo Kikuu cha Kentucky nchini Uingereza, ambaye pia ni mtalaamu wa afya ya akili kwa wasomi, anasema tafiti hiyo inaonesha namna mazingira ya kazi kwenye taaluma inavyochangia utulivu au matatizo ya akili kwa wanafunzi wa PhD.
Kila mwaka, maelfu ya watu duniani huvaa majoho na kwenda kutunukiwa shahada zao za uzamivu (Ph.D.) Kwa wengi, sherehe hizi zinafata baada ya mtu kuwekeza miaka kadhaa ya kusoma kwa bidii, kukabiliana na msongo wa mawazo unaotokana na ugumu wa masomo na kudaiwa ada.
Wengine wanaibuka tu siku hiyo ya kuhitimu na majoho yao bila kupitia tabu yoyote ya kimasomo ambayo wenzao wameipitia mpaka kustahili kuvalishwa majoho hayo na kuhitimu shahada zao. Wakiungana na wanafunzi hao, wanamichezo waliowahi kuwa na sifa ulimwenguni pamoja na wafanyabiashara mashuhuri au Marais wa nchi kama — Jakaya Kikwete, Mike Tyson, Oprah na Bill Gates — wameonekana kwenye vyuo mbalimbali wakipokea shahada ya “heshima” ya uzamivu.
Tofauti na wanafunzi waliosoma kupata elimu zao, watu hawa ambao ni kioo kwa jamii hutunukiwa shahada hizi bure kabisa: vyuo vikuu huwaruhusu kuuepuka utaratibu wote wa masomo unaotakiwa kumuwezesha mtu kupata shahada hii. Ingawa shahada hizi ni za heshima tu, na si kimatumizi, swala la watu kupewa shahada hizi halikuanza hivi karibuni.
Chuo Kikuu kutoa shahada ya heshima kwa mtu ni ishara ya chuo hicho kuonesha ishara ya kutambua mafanikio ya juu kabisa yaliyopatikana kwenye sekta, tasnia au nchi kutokana na mchango wa mtu husika. Chuo husika pamoja na jamii nzima vinatakiwa kuitambua shahada hiyo kama uthibitisho wa mafanikio ya mtu.
Shahada ya heshima inatunukiwa kutokana na mafanikio makubwa kabisa yaliyopatikana kutokana na mchango wa mtu fulani, hasa inapothibitika kuwa mchango wa mtu huyo katika taaluma, sekta au nchi husika ni mkubwa zaidi ya mchango ambao watu wenye taaluma hiyo wanaweza kuutoa. Hata hivyo, shahada hizi hazitunukiwi kwa watu kwa sababu za kisiasa au kiwango cha utajiri cha mtu.
Miongoni mwa sababu zinazoweza kufanya mtu atunukiwe shahada ya heshima na Chuo Kikuu:
Kwakuwa vyuo vikuu vina uhusiano wa karibu na jamii, ni jambo la busara kwao kutoa shahada za heshima kwa watu walioonesha kutambua mchango wa chuo husika kwa jamii. Mtu anayetunukiwa shahada ya heshima lazima awe anaunga mkono malengo na mchango wa chuo hicho kwenye jamii.
Shahada hii inaweza kutunukiwa kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa kwa chuo au jamii, ingawa yawezekana mtu huyo asiwe mashuhuri.
Miongoni mwa sababu zinazoweza kufanya mtu atunukiwe shahada ya heshima na Chuo Kikuu:
Kwakuwa vyuo vikuu vina uhusiano wa karibu na jamii, ni jambo la busara kwao kutoa shahada za heshima kwa watu walioonesha kutambua mchango wa chuo husika kwa jamii. Mtu anayetunukiwa shahada ya heshima lazima awe anaunga mkono malengo na mchango wa chuo hicho kwenye jamii.
Shahada hii inaweza kutunukiwa kwa mtu aliyetoa mchango mkubwa kwa chuo au jamii, ingawa yawezekana mtu huyo asiwe mashuhuri.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.