Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2018-01-16-00-52-04.png
 
Hakikisha unapotumia pasi usiiache ikiwaka ukande kufanya kazi nyingine. Pia vifaa vingine kama jiko la umeme, hita, hakikisha unazitoa au kuzima swichi mara baada ya kuzitumia ndipo uendelee na mambo mengine.
 
Epuka kutumia ‘extension cables’ kwa kudumu. Zitumike kw adharura na pia usiziweke kwenye mazulia.
 
Usiweke mapazia marefu dirishani yanayofunika soketi za umeme. Ni heri kuihamisha ikaka sehemu ya wazi kuliko kuifunika na pazia.
 
Makochi ndani ya nyumba yako na samani nyingine za ndani zisigusane na swichi au soketi yeyote ili isiwe rahisi kushika moto tatizo linapotokea. Ziweke angalau umbali wa inchi sita.
 
Kama fyuzi ya umeme itakatika au soketi breka itajizima yenyewe, hakikisha umemuita fundi kuja kukagua tatizo. Usiweke fyuzi nyingine au kuwasha soketi breka.
 
Hakikisha unamuita mkandarasi aliyesajiliwa kupitia mfumo wote wa umeme kwenye nyumba hasa maungio kila baada ya miaka mitano.
 
Usiongoze vitu vinavyotumia umeme mwingi kama viyoyozi bila kuwahusisha wakandarasi waliosajiliwa kuangalia uwezo wa umeme wako kuhimili mzigo unaouongeza.
 
Back
Top Bottom