Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

6. Kuathirika kisaikolojia;
Hakuna mwanamke ambaye hatakaa ajutie maamuzi yake ya kutoa mimba siku za usoni hata kama hakupata madhara yeyote hii itamfanya aishi kama ana deni Fulani maisha yake yote na itakua inamuumiza usiku na mchana. Zingine ni kukosa hamu ya kula, kusikia sauti ya mtoto anayelia wakati hayupo, kua na hasira sana…
 
0169ee84b64faa34654b6618dcb7e843.jpg
 
*UJUMBE WA ASUBUHI*


*BILA YA UVUMILIVU, UTAVUNJA NDOA KILA MARA....*

Ukiwa mtu wa kuangalia mambo kwa juu juu basi kila kitu kwako kitakuwa kigumu. Kusoma unaweza kuona ni kugumu, kufanya kazi kugumu, hata kusubiri mshahara unaweza kuona ni kugumu.
Urahisi kwako unaweza kuwa katika kutumia pesa, pengine na kula tu. Ila watu waerevu na wenye uvumilivu kwako kila kitu kinaweza kuwa tofauti na wewe.

Mahusiano yaliyodumu si kwa kuwa wahusika hawakoseani au makosa wanayokoseana ni madogo sana. Hapana. Kila binaadamu ana mapungufu yake. Wote huwa wanakoseana ila tofauti yake na wengine ni kwamba busara na uvumilivu huwa msingi wa mapenzi yao na ndiyo maana tunaona wanadumu mpaka leo.

Ni binaadamu gani unaweza kuishi naye na msikosane? Ni nani mwenye uwezo wa kukupa unachotaka kila siku? Hakuna binaadamu wa aina hiyo.

Mapenzi yasiyo kuwa na uvumilivu ndani yake hayana maisha marefu. Kwa sababu binaadamu ni kiumbe mwenye kukosea.



*Kumbuka,* siku zote wanaovumilia ndiyo huwa wanabaki na ushindi.Bila uvumilivu Mandela asingekuja kuwa raisi wa afrika kusini.Uvumilivu ni kila kitu katika maisha.

*JUMAPILI YA TRH 21 JAN 2018*
 
Back
Top Bottom