Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

210bb38c44961908f60ba2f080d892be.jpg
 
Mfugaji alinung'unika sana lakini alimbidi akubaline na hali hiyo ambayo imetokea. Hivyo akaamua kumuhudumia yule ng'ombe kama mtoto wake kwani kila alichokihitaji ng'ombe yule alikipata kutoka kwa mfugaji huyo. Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya mfugaji na ng'ombe yalivyokuwa.
 
Kwa maendeleo ya nchi yeyote, rasilimali watu ni kitu cha muhimu sana. Ukiwa na miundombinu mizuri na hospitali nzuri kama nchi inaupungufu wa watu ni changamoto kubwa sana.
 
Kufuatia hatua hiyo, mataifa 9 duniani yamewashauri wananchi wake kuzaa watoto zaidi kutokana na upungufu wa watoto katika mataifa hayo.
 
Denmark
Nchini Denmark wananchi wake wameambiwa kuwa hata kama hawana mpango wa kuwa na watoto kwa ajili ya famili zao wenyewe, basi wazae japo kwa ajili ya nchi ili kuongeza idadi ya watu.
 
Urusi
Nchini Urusi wanaume wengi hufariki wakiwa vijana. Ugonjwa wa UKIMWI na unywaji pombe kupindukia unasababisha vifo na hata kupoteza nguvu za kiume kitu kinachopelekea wanawake kushindwa kuzaa.
 
Tatizo hili lilikuwa kubwa kiasi cha mwaka 2007 Urusi kutangaza kuwa Septemba 12 ni siku ya kutafuta watoto. Siku hiyo wazazi hawaendi kazini na hubaki nyumbani kujamiiana ili kupata watoto. Atakayezaa mtoto baada ya miezi 9 toka siku hiyo anazawadiwa friji.
 
Japan
Japan imekumbwa na matatizo ya uzazi tangu mwaka 1975. Mwana 2010 wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Tsukuba walitengeneza roboti mtoto ambaye hupewa wazazi ambao hawana mtoto wakiamini kuwa wakikaa na roboti huyo kama mtoto watashawishika kupata mtoto wa kweli.
 
Romania
Miaka ya 1960 Romania ilikumbwa na tatizo la uzazi ambapo serikali ilifikia uamuzi wa kuweka kodi ya asilimia 20 kwa wapenzi wasio na mtoto na kuweka kifungu cha sheria kilichokuwa kikifanya utoaji talaka kuwa mgumu.
Hizi zote ni jitihada za kuhakikisha kuwa idadi ya watu inaongezeka.
 
Singapore
Kutokana na upungufu wa watu nchini Singapore, serikali ya nchi hiyo imeweka vizuizi kwa nyumba za kulala wageni au hoteli kuwa na vyumba vingi vya kulala mtu mmoja mmoja. Hi ni kuta kuwepo ongezeko la watu kuweza kulala wawili wawili.
 
India
Nchi nzima ya India kwa ujumla haina upungufu wa wa watu. Lakini watu wa jamii ya Parsis wanapungua kwa kasi. Watu wa jamii hiyo wamepungua kutoka 114,000 mwaka 1941 hadi 61,000 mwaka 2001.
 
Kufuatia hali hiyo, serikali ya India imekuwa imkiwataka watu wa jamii hiyo kutotumia mipira ya kiume au ya kike (condoms) wakijamiiana usiku. Pia imeendeshwa kampeni ya kutaka vijana kujitegemea na kuacha kuishi na wazazi wao. Hii imechangia kuongezeka kwa watu hadi 69,000.
 
Back
Top Bottom