Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usichelewe kwenda haja.
Kutunza mkojo kweye kibofu chako kwa muda mrefu ni wazo baya. Kibofu kikijaa kinaweza kusababisha uharibifu. Mkojo ambao unakaa kwenye kibofu huzidisha bakteria haraka. Mara mkojo unaporudi nyuma ya njia na Figo, sumu dutu husababisha maambukizi ya figo, pia njia ya mkojo na "nephritis", pamoja na "uremia". Wakati wito asili (unahisi mkojo) fanya hivyo haraka iwezekanavyo.
 
Kula nyama nyekundu kupita kiasi.
Protini ikizidi sana katika mlo wako inadhuru figo zako. Mmeng'enyo wa Protini unazalisha amonia- sumu dutu ambayo ina uharibifu mkubwa kwa figo zako. Nyama nyingi inaleta uharibifu zaidi wa figo.
 
Unywaji mwingi wa "Caffeins".
Caffein hutokana na vinywaji vya Soda na vinywaji vingine laini kama Kahawa, Redblue n.k. Hupandisha shinikizo la damu na figo zako kuanza mateso. Unapaswa kupunguza kiwango cha Coke, Pepsi, Red Bull, nk ambavyo hunywa kila siku.
 
Kutokunywa maji.
Figo zetu lazima zichakatwe vizuri kutekeleza majukumu yake vizuri. Endapo hatunywi ya kutosha, sumu dutu inaweza kuanza kukusanyika katika damu, kama hakuna kimiminika cha kutosha kutoa kwa njia ya figo. Inashauriwa Kunywa zaidi ya bilauri 10 za maji kila siku. Kuna njia rahisi ya kuangalia kama unakunywa maji ya kutosha. Angalia rangi ya mkojo wako; Wepesi wa rangi, ndiyo vzuri.
 
Bizari (Turmeric) ni kiungo cha mboga jamii ya mimea unaochimbwa kama mizizi, mfano wa tangawizi, lakini tangawizi yenyewe ina rangi ya njano na hujulikana pia kama ‘manjano’ kutokana na rangi yake.
 
Kiungo hiki kinatumiwa sana katika Bara la Asia na hasa India na China. Kutokana na umuhimu wake kiafya, vyakula vingi hupikwa kwa kuchanganya na kiungo hiki ambacho sasa kimeenea dunia nzima, ikiwemo Tanzania.
 
FAIDA ZA BIZARI KIAFYA
Bizari hutumika na watu wengi kama kiungo cha mboga cha kuongeza ladha katika mchuzi na pengine kuweka rangi, lakini kuna faida nyingi unazozipata unapotumia kiungo hiki kila mara katika mapishi yako.
 
Inaelezwa kuwa bizari ina virutubisho vyenye uwezo wa kuimarisha kinga ya mwili, mara 8 zaidi ya Vitamin C na Vitamin E, ina uwezo wa kushusha kiwango cha lehemu (cholesterol) na kuzuia mtu kuzeeka kabla ya wakati.
 
Aidha, bizari huimarisha sehemu za magoti hivyo kukuepusha na matatizo ya miguu kuuma. Bizari pia hun’garisha ngozi na kuifanya kuwa yenye afya na huimarisha pia mfumo wa usagaji chakula (Digestion
 
SUALA LA UBORA NI MUHIMU
Katika ulimwengu wa maendeleo ya sayansi na teknolijia tulionao sasa, bizari hutengenezwa viwandani na kuhifadhiwa kwa usafirishaji sehemu mbalimbali duniani na kwa ajili ya matumizi ya muda mrefu. Katika hali kama hiyo, si ajabu kukuta bizari iliyoongezewa kemikali zingine za kuhifahdia chakula.
 
Bizari ya aina hiyo, tayari inakosa faida zilizoelezwa hapo juu, hivyo ni suala muhimu kuangalia ubora wa bizari unayoitumia na mahali inapotoka. Katika nchi yetu, Mungu ametujaalia ardhi yenye rutuba ambapo kiungo kama hiki kinalimwa na kupatikana kwa wingi na kwa uhalisia wake.
 
Katika suala la kujali ubora, pendelea zaidi kununua bizari kutoka sokoni ambayo imetengenezwa katika mazingira safi na salama na bila kuchanganywa na kitu kingine. Iwapo pia utanunua bizari iliyokwisha hifadhiwa, ni vyema ukasoma maelezo yake kuona kama haina vikorombwezo (additives) vingine.
 
Ni ukweli ulio wazi kuwa ukitumia bizari iliyobora utapa faida nyingi kiafya, hivyo hakikisha katika upikaji wako wa kitoweo cha nyama, kama vile kuku, samaki, ngo’mbe unaweka bizari. Upikaji mzuri ni ule wa kuweka kiungo hicho mwisho baada ya mboga yako kuchemka na kuiva, kwani haitakiwi bizari kuchemka sana.
Kwa ujumla hizi ndizo faida utakazozipata ukiifanya bizari kuwa sehemu ya viungo katika mlo wako wa kila siku:
 
Ni ukweli ulio wazi kuwa ukitumia bizari iliyobora utapa faida nyingi kiafya, hivyo hakikisha katika upikaji wako wa kitoweo cha nyama, kama vile kuku, samaki, ngo’mbe unaweka bizari. Upikaji mzuri ni ule wa kuweka kiungo hicho mwisho baada ya mboga yako kuchemka na kuiva, kwani haitakiwi bizari kuchemka sana.
Kwa ujumla hizi ndizo faida utakazozipata ukiifanya bizari kuwa sehemu ya viungo katika mlo wako wa kila siku:
 
UTAIMARISHA KINGA YA MWILI WAKO
UTAIMARISHA AFYA YA MACHO
UTAIMARISHA SEHEMU ZA VIUNGIO VYA MWILI WAKO
UTAIMARISHA UTENDAJI KAZI WA INI
UTAIMARISHA CHEMBE HAI ZA MWILI
UTAIMARISHA MFUMO WA USAGAJI CHAKULA
UTAIMARISHA MFUMO WA DAMU MWILINI
 
Back
Top Bottom