Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Januari 2016, mwanamke mmoja jimbo la Madhya Pradesh katikati mwa nchi hiyo aliumia vibaya begani baada ya kipande kikubwa cha barafu kutoka angani kuangukia nyumba yake.
Gazeti moja lilisema huenda aligongwa na kipande cha kinyesi kilichokuwa kimeganda.
 
Kinyesi kutoka kwenye ndege ambacho kimeganda mara nyingi huitwa "barafu ya buluu" kwa sababu ya kemikali ambazo huongezwa kupunguza uvundo na kuyeyusha uchafu huo.
Shirika la uchukuzi wa ndege Uingereza linasema visa vya kaunguka kwa "barafu ya buluu" 25 huripotiwa kila mwaka kutoka kwa safari 2.5 milioni za ndege ambazo hufanywa katika anga ya Uingereza kila mwaka.
 
Nyota wa zamani wa kandanda duniani George Opong Weah ameapishwa kuwa rais wa Liberia katika sherehe iliyohudhuriwa na maelfu ya watu katika mji mkuu Monrovia.
Weah amechukua nafasi ya rais wa kwanza mwanamke kuwahi kuchaguliwa kuongoza taifa la Afrika Ellen Johnson Sirleaf, ambaye amestaafu.
 
Kuingia kwa Weah madarakani kunakamilisha shughuli ya kwanza ya amani ya mpito nchini humo tangu mwaka 1944.
Sherehe hiyo imehudhuriwa na viongozi wa mataifa kadha pamoja na nyota wa kandanda duniani.
Akihutubu baada ya kula kiapo, Bw Weah amesema: "Nimekuwa katika viwanja vingi maishani, lakini sijawahi kuhisi hivi."
 
Bw Weah ameahidi kujitolea kuwatumikia raia wa nchi hiyo.
"Nitafanya zaidi ya mchango ninaotarajiwa kutoa ili kutimiza matarajio yenu - lakini naomba nanyi mtimize matarajio yangu, siwezi kutimiza haya peke yangu."
 
Kiongozi huyo ametumia hotuba yake kusifu uhusiano wa karibu kati ya taifa hilo na Marekani na China.
Kadhalika, amezungumza kuhusu Umoja wa Ulaya.
Amesema: "Bila bara Ulaya, Weah hangekuwa amesimama hapa leo."
 
Weah alicheza mpira wa miguu katika klabu kadha za Ufaransa na Uingereza miaka ya 1980 na 1990 na akaibuka Mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya Fifa ya Mchezaji bora wa mwaka duniani na tuzo ya Ballon d'Or.
Didier Drogba kutoka Ivory Coast ni miongoni mwa wachezaji mashuhuri ambao wamehudhuria sherehe hiyo katika uwanja wa Samuel Doe viungani mwa mji wa Monrovia.
 
-618565603526619977.jpg
 
Weah aliingia katika siasa baada ya kustaafu soka mwaka 2002 na akawa miongoni mwa maseneta katika bunge la Liberia.
Aligombea urais mwaka 2005, na alimshinda Bi Johnson Sirleaf wakati wa duru ya kwanza katika uchaguzi huo lakini akashindwa katika duru ya pili ambapo kambi yake ilisusia kushiriki katika duru ya pili.
 
Mambo saba muhimu kumhusu George Weah:
Alizaliwa mnamo 1 Oktoba, 1966, na akalelewa katika mtaa wa mabanda Monrovia
Alinunuliwa na Arsene Wenger kuchezea Monaco kutoka klabu ya Tonnerre Yaoundé ya Cameroon
Alichezea Monaco mechi yake ya kwanza 1987, na baadaye akachezea AC Milan, Paris Saint-Germain na Chelsea
Ndiye Mwafrika pekee aliyewahi kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani ya Fifa
Aliwania urais mara ya kwanza 2005, na akashindwa na Ellen Johnson Sirleaf
Alifuzu na shahada ya biashara kutoka chuo kikuu kimoja cha Marekani, baada ya kudaiwa hakuwa na elimu
Alichaguliwa rais Desemba 2017
 
Back
Top Bottom