Mambo saba muhimu kumhusu George Weah:
Alizaliwa mnamo 1 Oktoba, 1966, na akalelewa katika mtaa wa mabanda Monrovia
Alinunuliwa na Arsene Wenger kuchezea Monaco kutoka klabu ya Tonnerre Yaoundé ya Cameroon
Alichezea Monaco mechi yake ya kwanza 1987, na baadaye akachezea AC Milan, Paris Saint-Germain na Chelsea
Ndiye Mwafrika pekee aliyewahi kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani ya Fifa
Aliwania urais mara ya kwanza 2005, na akashindwa na Ellen Johnson Sirleaf
Alifuzu na shahada ya biashara kutoka chuo kikuu kimoja cha Marekani, baada ya kudaiwa hakuwa na elimu
Alichaguliwa rais Desemba 2017