Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Anza sasa kuwaza mambo makubwa ili uwe mtu mwenye ndoto njema ya maendeleo.
Kutokana na hali hiyo ya watu kujikatisha tamaa, wale ambao wamewahi kufanya biashara na kufilisika, wengi wao wamekuwa wakisema kuwa hawatarudia tena kufanya biashara hiyo.
 
Lakini kumbe, haikuwapasa kukata tamaa, bali kujipa moyo, na kuelewa kuwa pamoja na hali hiyo ya kushindwa inawapasa kujaribu tena.
Kamwe usikate tamaa katika jambo lolote unaloliwaza ama kulifanya. Kwa kuwa, upo msemo mmoja unaosema, penye nia pana njia.
 
Kitu muhimu zaidi katika maisha ya binadamu ni mahusiano – Familia, Marafiki na Wapenzi. Familia hubakia na wewe mara zote, Wenzi wa maishani tunapewa nafasi ya kuwachagua na kwa hili wengine hubahatika zaidi katika kila kitu, yaani kuwa na mahusiano mazuri na kila mtu anayemzunguka maishani, na wengine ikawa sivyo.
 
Tunafanyaje endapo watu wetu wa karibu wameamua kututelekeza au kutuumiza kwa aina yoyote? Kujenga chuki, kupata msongo wa mawazo ni kawaida ila kumbuka kila jambo linalotokea katika maisha yako lazima likuache na fundisho lolote licha ya kuwa umeumia nah ii si kwako tu,
 
hata kwa yule aliyeamua kukutenda kwa lolote. Ni tabia ya kibinadamu kuendelea kufikiria mahusiano yoyote yaliyokwisha, na huchukua muda sana kujua kwamba huwezi kuongoza kila jambo katika maisha yako na sio vyema kupeleka lawama kwa wengine.
 
1. Kubaliana na mabadiliko: Maana ndio kitu pekee kitakachokua sawa kwenye maisha yako. Kila mahusiano lazima yapitie mabadiliko, inawezekana mabadiliko hayo yakawa ya muda mfupi, ya muda mrefu au hata ya moja kwa moja, ni vizuri ukaamua kukubaliana na mabadiliko hayo kwa mikono yote miwili.
 
2. Wakati huponya kila donda: Jipe muda wa kupoa, wakati unauwezo wa kuleta yote mazuri na mbaya na wakati huo huo unauwezo wa kuponya kila kitu katika maisha. Vuta subira na subiri wakati wako wenye faraja tena.
 
3. Maisha yanaendelea siku zote: Maisha hayasimami kamwe kisa tu kuna mtu ameondoka au ameingia kwenye maisha yako. Ukiumizwa unatakiwa kujifunza kuishi na maumivu ya moyo mpaka siku utakaposahau au, na hicho ndo kitakachokufanya wewe uonekane ni jasiri na mwenye kuelewa maisha.
 
4. Kila mtu ana vipaumbele vyake maishani: Kila mtu ana dondo zake, na wakati mwingine watu huamua kufanya maamuzi magumu nap engine yakawa ni ya kibinafsi ili tu atomize ndoto zake na siku zote itaonekana ni maamuzi mabya kwa watu wengine lakini kiukweli hakuna baya kwa mtu kujitakia maisha mazuri au ya aina Fulani hata kama wewe haupo kwenye maisha hayo.
 
5. Jifunze kuachana na vitu ambavyo hauna uwezo wa kuvi-control: Sio kila kitu unaweza kukiongoza hata kama unafedha kiasi gani, kamwe usiwaze kuwa watu wako wa karibu hawatakjaribu kukuacha kisa una kitu, ndoto za watu ni muhimu sana maishani mwao na wala usijaribu kutumia kigezo hicho kuwalazimisha. Usije ukawa sababu ya mtu kutokua na furaha au Amani.
 
6. Wengine huwa hawaondoki patupu, daima huacha makovu kwenye maisha yako: Akiondoka anaondoka kimwili na kwamba ndio utakua humuoni tena kama ilivyokua nyuma lakini vyote mlivyokua mkifanya pamoja, mkacheka na pengine hata alikufundisha kitu muhimu sana maishani. Kamwe hutasahau na hivyo ndivyo atakavyokua anaishia ndani yako milele.
 
Back
Top Bottom