Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuajiri na kuwapa vyeo wafanyakazi wasiostahili
Wafanyakazi wazuri na wenye juhudi wanapenda kufanya kazi na watu wanaofanana au waliowazidi uwezo. Endapo mabosi watazembea na kujikuta wanaajiri watu wenye uwezo mdogo, itafanya wafanyakazi wazuri kukosa msukumo wa kiushindani na kutoweka juhudi kazini.
 
Kuwapa vyeo watu wasiostahili au wenye uwezo mdogo ndio jambo baya zaidi. Kama unafanya kazi kwa ubunifu na uwezo wako wote na unaachwa kila msimu wa kupandishwa vyeo unapowadia na vyeo hivyo kupewa watu wenye uwezo mdogo zaidi ya ulionao, bila shaka utaona umedharauliwa kupita kiasi na yawezekana kabisa moja ya maamuzi utakayofikiria kuyafanya ni kuacha kazi hiyo.
 
Kutoruhusu wafanyakazi wao kufanya kazi wanayopenda

Wafanyakazi wenye vipaji na uwezo mkubwa huwa hawalazimishwi kufanya kazi, huwa wanajituma wenyewe. Kuwapa nafasi ya kufanya kazi kwa uhuru ili watumie ubunifu wao huwafanya waridhike.
 
Lakini mabosi wengi wananataka watu wafanye kazi kwenye mazingira ya woga. Mabosi wa aina hii wanakuwa na hofu kwamba uzalishaji wa kampuni zao utapungua endapo watawaruhusu wafanyakazi wao wafanye mambo wanayoyapenda.
 
Kushindwa kuwaongezea watu mbinu bora za kufanya kazi
Pindi mabosi wanapoulizwa kuhusu mambo wasiyoyajua kuhusu wafanyakazi wao, wengi huwa wanatoa visingizio kama: “nawaamini,” “nimewapa uhuru kwenye kazi zao,” na “nawawezesha kujitegemea.”
 
Hili ni suala baya kwakuwa mabosi wazuri huwa wanafatilia kila jambo kwa karibu na umakini, bila kujali mfanyakazi ana kipaji au uwezo mkubwa kiasi gani. Wanasikiliza wafanyakazi wao muda wote na kuwaambia athari ya kila wanachokifanya.
 
Ukiwa na wafanyakazi wenye vipaji au uwezo mkubwa, ni jukumu lako kama bosi kuwaangalia kwa umakini na kuwashauri wanapoweza kufanya maboresho ili waweze kupata matokeo bora zaidi. Wafanyakazi wenye uwezo mkubwa wanapenda wapewe mrejesho wa kazi wanayofanya — mara nyingi zaidi ya wale wenye uwezo mdogo au wa kawaida — na ni jukumu lako kama bosi wao kuwapa mrejesho huu. Kama hutafanya hivi, wafanyakazi wako wenye uwezo zaidi wataichukia kazi na hatimaye kukukimbia.
 
Kushindwa kutumia ubunifu wa wafanyakazi wao
Wafanyakazi wengi wenye vipaji, ubunifu na uwezo mkubwa zaidi huwa wanataka kuboresha kila kitu kwenye maisha yao. Kama ukiwaweka kwenye mazingira ambayo uwezo na ubunifu wao hauwezi kutumika kwa kiwango cha juu kwa sababu unaridhishwa na hali ya sasa, itawafanya waanze kuchukia ajira zao. Kuwazuia wasifanye ubunifu wao ni hakuathiri utendaji kazi wao tu, bali inaathiri utendaji wa taasisi au kampuni yako pia.
 
Kushindwa kuwapa wafanyakazi wao changamoto za kutosha
Mabosi wazuri wanawapa wafanyakazi wao changamoto ya kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuweza kufikia malengo ambayo mwanzo yawezekana yalionekana ni makubwa kupita kiasi na yasiyoweza kutimia. Badala ya kuweka malengo mengi madogo madogo, wao wanaweka malengo makubwa sana yanayofanya wajitume zaidi ya walivyokuwa wanafanya kabla.
 
Hivyo basi, ni wazi kuwa mabosi wazuri wanafanya kila jitihada zilizo ndani ya uwezo wao kuwasaidia wafanyakazi wao wapate mafanikio kwakuwa wafanyakazi wenye uwezo mkubwa kazini wanapojikuta wanafanya kazi nyepesi zisizo na changamoto kwao, watajikuta wanatafuta ajira sehemu nyingine ambazo zitawafanya watumie uwezo wao vizuri.
 
Kama unataka wachapakazi wako wabaki, yakupasa kufikiria vizuri na kuwa na mkakati wa kuwafanya wabaki kazini. Kwakuwa wafanyakazi wazuri huwa ni watu wenye msimamo sana na vipaji vyao vinawafanya wawe na wigo mpana wa kuchagua kazi, ni kazi yako kama bosi kuwafanya wapende kubaki na kufanya kazi na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…