Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

e8674617ef25919027b0e2350f2588af.jpg
 
purs watashuka dimbani wakiwa na kumbukumbu ya kupata sare katika mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Southampton.

Kikosi hicho cha kocha Mauricio Pochettino, kinashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi, kikiwa kimeshajikusanyia pointi 45.
 
Kwa upande wa Man United, wao wataingia kuzisaka pointi tatu wakiwa na nguvu ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Yeovil Town katika mtanange wa Kombe la FA.

Mourinho na vijana wake wako nafasi ya pili nyuma ya Man City, wakiwa na pointi 53 walizozivuna katika mechi 24.
 
Vita inaanzia hapa

Mtanange wa leo ni muhimu kwa timu zote na hilo ndilo litakaloufanya uwe mkali na unaovutia kuutazama.

Spurs wenye pointi 45, watahitaji ushindi ili kuingia ‘top four’, nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Liverpool.
 
Lakini pia, Man United watakapopoteza leo, basi watakuwa wamepunguziwa kasi ya kuwakimbiza Man City walio kileleni mwa msimamo kwa tofauti ya pointi 12.

Mbali na hilo, watakuwa wameiweka rehani nafasi yao ya pili ambayo inanyemelewa na Chelsea.
 
Rekodi za nyumbani, ugenini

Licha ya kwamba Spurs watakuwa nyumbani, wasitarajie mteremko kwa Man United. Watambue kuwa Mashetani Wekundu hao wameshacheza mechi 12 za ugenini msimu huu na wameshinda saba na kutoa sare tatu.
 
Lakini pia, Man United nao wasichukulie poa kwani Spurs wamekuwa hatari zaidi wanapokuwa nyumbani katika Uwanja wa Wembley.

Katika mechi 12 walizocheza mbele ya mashabiki wao msimu huu, wameshinda saba, wakatoa sare nne, hivyo wamefungwa moja pekee.
 
Katika mechi tano zilizopita kwa kila timu hakuna iliyopoteza, Spurs wameshinda tatu na kutoa sare mbili, Man United wao wamechekelea ushindi mara mbili na kutoa sare tatu.
 
Back
Top Bottom