Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

58a135e804b455c0f5dc4016e4c78300.jpg
 
Kuna idadi kubwa ya watu wanatumia neno shikamoo kama sehemu ya kuonyesha heshima au salamu kwa mtu aliyekuzidi umri.
 
Ila ni muhimu sana tukaelewa maana na historia ya na maneno “Shikamioo” na “Marahaba”. Kama ifahamikavyo kuwa kila jambo huwa na mwanzo na mwanzo huwa na sababu za kufanya hilo jambo kuibuka.
 
Ni hivi kabla ya miaka ya 600 BK au BM, Wabantu walikuwa wameshafika Pwani ya Afrika mashariki. Na ukweli ni kwamba Wabantu walishapata kuishi hapo na hata wageni waliofika walikiri suala hilo. Na kwa kuwa Wabantu walipata kuishi hapo walikuwa na mitindo yao wa maisha na walikuwa wakiheshimiana.
 
Kikubwa zaidi Wabantu walikuwa na salamu zao. Kwa mfano Wazaramo (historia yao itaandikwa) walikuwa na salamu yao kama ifuatavyo, aliyekuwa akiamkia alionyoosha mikono mbele na kusema “simbamwenee” na kisha anayeamkia huitikia “utwaaa”. Na kila mtu alikuwa akifurahia salamu hiyo, iliyokuwa nzuri kuitamka mdomoni.
 
Lakini mambo yalibadilika pale walipokuja Waarabu na kuanzisha biashara ya utumwa. Na hapo tukapata makundi mawili yaani “mtumwa” na “bwana” na mtumwa alipaswa kumuamkia Bwana kwa neno la “Nashika Miuu” akiwa na maana ya “Nashika Miguu”. Na kila mtumwa alipaswa kujua na kutambua salamu hii.
 
Na mtumwa alipaswa kutoa salamu hii hata mara 100 kwa siku moja. Lengo la salamu hii ilikuwa ni kutenganisha kati ya mtumwa na bwana wake.
 
Na mtumwa alipaswa kutoa salamu hii hata mara 100 kwa siku moja. Lengo la salamu hii ilikuwa ni kutenganisha kati ya mtumwa na bwana wake.
 
Na kila walipofika salamu hii waliitumia na baadhi ya machifu waliipenda sana salamu hii. Na kujikuta wakiwa na matamshi tofauti juu ya salamu hiyo. Na kwa wakati wote huo ilikuwa ni salamu ilikuwa ni "Nashika Miuu" na sio "Shikamoo" kama ilivyo sasa.
 
Kuanzia miaka ya 600-1700, salamu hii ilikuwa ikitumika maeneo ya Pwani tu. Na kuanzia miaka ya 1700 mwishoni na 1800 mwanzoni Waarabu walianza kuingia maeneo ya ndani ya Afrika mashariki.
 
Kutokana na watu tofauti kutumia salamu hii, wapo waliotamka "Shikamuu" kama neno moja. Na mpaka miaka ya 1930, kipindi ambacho Kiswahili kinafanyiwa usanifishaji ndipo tukapata neno "shikamoo."
 
Na kuhusu neno "Marahaba", lina maana ya "asante". Na neno hili huitikiwa na Yule anaeamkiwa (Bwana) ambaye miguu yake imeshikwa na mtumwa. Na mpaka sasa salamu hii inatumiwa sana na Watanzania wengi licha ya kuwa na salamu zao za kikabila.

Hii ndio historia fupi ya neno "Shikamoo" na "Marahaba".
 
Mara nyingi tumezoea kuona mwanamke anapoolewa mahari ambazo hutolewa ni ng’ombe, mbuzi, fedha au vitu vingine vya kawaida ambavyo hutumika katika jamii kila siku, lakini kwa wakazi wa Mkoa wa Katavi wao hali ni tofauti.
 
Mwanaume wa Kabila la Wapimbwe waishio wilayani Mlele mkoani Katavi wanapooa hulazimika kutoa gobore kama sehemu ya mahari kwa wazazi wa mwanamke.
 
Mmoja wa wazee wa kabila hilo akielezea sababu ya kudai gobore kama sehemu ya mahari ni kwa sababu kabila hilo shughuli yao kubwa ni uwindaji, hivyo kudai gobore katika mahari ni ili kujiongezea zana za uwindaji. Aidha alisema kwa sasa hali hiyo imepungua kutokana na sheria kali za uwindaji na umiliki wa silaha.
 
Back
Top Bottom