Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Prosesa ni sehemu muhimu inayobana mambo mengi ikiwemo jinsi simu inavyomudu rangi, chaji ya betri na kasi ya kuendesha programu. Prosesa zinapambanishwa kwa kipimo cha GHz, ambapo namba kubwa zaidi inaonesha uwezo mkubwa na kasi zaidi.
 
Prosesa vinazotamba kwa kasi sasa hivi ni za Snapdragon, Exynos, A8 ya Apple na MediaTek. Na katika hizo, kuna aina nyingi: Quadcore Snapdragon 801, 805, Apple A7. Inafaa ulize ipi inayotamba sokoni kila wakati kwa sababu zinatengenezwa kwa kasi sana.
 
Unaponunua simu angalia uwezo wa kukaa na chaji(unaopimwa kwa mAh) na teknolojia ya betri. Betri za mhA 2000 na kuendelea zitakupa muda kuanzia masaa sita ya chaji ukiwa unaitumia simu sana. Chini ya hapo unahitaji uvumilivu wa kutosha wa kutembea na chaja au betri ya ziada au kujibanana.
 
Siku za karibuni, moja ya wakubwa wa Blackberry amekaririwa akilalamika kuhusu mfumo wake kukosa mvuto wa watengenezaji wa apps muhimu na hivyo kuleta wasiwasi kwa watumiaji wa Blackberry kubaki na mfumo huo. Ni jambo muhimu sasa kuangalia mfumo gani unakufaa na sifa zake.
 
Windows inasifiwa kwa kutengenezwa vizuri (‘hardware build’), Android inasifiwa kwa uhuru wa kuifanya utakavyo na kubadilisha muonekano wake utakavyo. Simu za Apple zinasifiwa kwa kuwa na kiwango na mvuto wa kipekee. Blackberry yenyewe inapendwa na wafuasi wake kwa sababu ya kibodi yake na upekee wa aina yake.
 
Ukubwa na Uhalisia wa Skrini

TFT, IPS, Retina Display na True HD ni majina machache ya mauzo kati ya majina ya skrini nyingi duniani. Je, unajua skrini bomba kwa sasa? – Jibu ni skrini yoyote yenye ukubwa wa kuanzia inchi 4.5! Hili ni kutokana na wachambuzi wengi na hata ukiiangalia simu zinazoingia sokoni sasa hivi. Watu wanataka kuona kioo kikubwa, siyo kuchungulia skrini tena.
 
Upya wa simu

Watu wengine huchagua simu kutokana na sifa ya upya. Sabababu kuu ikiwa ni za kujijengea jina. Endelea kufuatilia makala zetu hapa teknokona Tutakutangazia na kukuletea uchambuzi wa simu bomba, kwanza.
 
Back
Top Bottom