Kampeni kubwa imesambaa duniani wakati dunia leo inaadhimisha siku ya saratani duniani - [HASHTAG]#WorldCancerDay[/HASHTAG] - kupiga vita saratani kwa kuongeza uhamasisho kuhusu umuhimu wa kutambua mapema na kuzuia kusambaa kwa saratani.
Shirika la afya duniani WHO linasema saratani ndio chanzo cha kifo cha mtu mmoja kati ya sita duniani, na hadi 50% ya aina zote za saratani zinaweza kuzuilika.
Saratani ya matiti inaongezeka, hususan katika mataifa yanayoendelea, ambapo visa vingi hutambuliwa katika awamu ya mwisho wakati ugonjwa tayari umesambaa mwilini mwa muathiriwa.