Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

27581687_185008818926807_246509201277321216_n.jpg
 
Gazeti hilo limechapisha pole kwa Wanjigi likisema litafanya kila juhudi kuhakikisha wahalifu wananaswa na mkono mrefu wa sheria. Kama nilivyosema hapo awali, Wanjigi hana imani na uchunguzi wa polisi na pengine anapanga kuanzisha uchunguzi wake akitumia wachunguzi wa kibinafsi.
 
Inaeleweka kwa nini Wanjigi hana imani kwa polisi. Anasema Jubilee inawatumia kumhangaisha na kumyima haki zake za kibinadamu.

Juzi Serikali ilitangaza kuwa viongozi wote wa Nasa akiwemo Wanjigi wanatakiwa kurejesha hati zao za kusafiria idara ya uhamiaji na usajili wa watu kabla ya siku 21 kumalizika.
 
Uamuzi huo unalenga kuwazuia viongozi hao kuzuru nchi za ughaibuni. Tayari, Serikali ilimpokonya hati ya kusafiria mwanasiasa wa kitengo cha Nasa cha National Resistance Movement (NRM), Miguna Miguna ambaye Februari 5 alisafirshwa kwenda Canada kwa maelezo ni raia wa huko. Miguna alilakiwa kwa shangwe na umati wa wafuasi wa Nasa nchini humo kwenye uwanja wa ndege jijini Toronto.
 
Miguna ambaye alijitwika wadhifa wa jemedari kwenye NRM, bado hajaacha ndoto yake ya kupinga Jubilee. Ananuia kurejea nchini Kenya hivi karibuni kuendeleza mchakato wa kuondoa Jubilee madarakani.

Wanjigi kama Miguna, anajua Jubilee imemweka kwenye darubini na ataachwa tu ikiwa ataachana na Nasa na siasa za NRM.
 
Kama mtu aliyekata shauri kuhusu anachotaka kufanya bila kujali yanayoweza kumpata, Wanjigi anasema ataendelea kusukuma harakati za kuhakikisha hakutakuwa na wizi wa kura nchini nchini humo.

Wanasiasa wengine wa Nasa kama vile aliyekuwa seneta wa Machakos, Johnsone Muthama, Seneta wa Kaunti ya Siaya, James Orengo wamekaidi amri ya Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’I ya kuwataka warudishe pasipoti zao.
 
Alipoulizwa kwa nini Miguna alifukuzwa, Matiang’I alijibu: “Tumeirejeshea Canada mwananchi wake.”

Miguna ana uraia wa nchini mbili, Canada na Kenya ambayo ni nchi yake ya kuzaliwa. Katiba ya Kenya inaruhusu uraia wa nchini mbili.

Ni vigumu kuelewa ni sheria gani iliyotumiwa kumfukuza Miguna lakini ukweli ni kwamba sheria hiyo kama ipo, haiko kwenye Katiba.
 
Alipoulizwa kwa nini Miguna alifukuzwa, Matiang’I alijibu: “Tumeirejeshea Canada mwananchi wake.”

Miguna ana uraia wa nchini mbili, Canada na Kenya ambayo ni nchi yake ya kuzaliwa. Katiba ya Kenya inaruhusu uraia wa nchini mbili.

Ni vigumu kuelewa ni sheria gani iliyotumiwa kumfukuza Miguna lakini ukweli ni kwamba sheria hiyo kama ipo, haiko kwenye Katiba.
 
Licha ya Wanjigi kutangazwa kuwa ameenda kukutana na muumba wake, hii si mwisho wa makabiliano yake na Serikali. Mengi yanatarajiwa huku ikiaminika kwamba Matiang’I anapanga kuwanasa viongozi wa Nasa.

Kwa kuhofia kunaswa kama vile Miguna alivyonaswa, baadhi ya viongozi wa Nasa walijipeleka kituo cha jinai Nairobi kupata kibali cha kutonaswa.
 
Makamu wa Rais, William Ruto amesema hakuna mazungumzo yoyote kuhusu kura yatakayofanyika kama vile Nasa inataka.

“Mazungumzo ninayotarajia kati ya Serikali na Nasa ni yale yanayolenga jinsi ya kuimarisha uchumi wetu,” anasema Ruto kwenye mazishi ya mjane wa aliyekuwa makamu wa rais, marehemu Michael Wamalwa, Yvonne.
 
Back
Top Bottom