Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jina la Pasifiki (kwa Kilatini: yenye amani, yaani kimya) limetokana na Wazungu wa kwanza waliovuka bahari hii mwaka 1520 BK kutoka Amerika ya Kusini hadi Ufilipino wakaikuta kuwa ni bahari tulivu.
 
6b3ef8cf50da03c808781700c945cf9b.jpg
 
Atlantiki ni bahari kubwa inayotenganisha Amerika upande wa magharibi na Afrika na Ulaya upande wa mashariki. Eneo lake ni kilometa za mraba 106,200,000 au sehemu ya tano ya uso wa dunia pamoja na bahari za pembeni kama bahari ya Baltiki na Mediteranea. Hivyo ni bahari kubwa ya pili duniani baada ya Pasifiki. Bila bahari hizi za pembeni eneo lake ni kilometa za mraba 82,400,000.
 
Beseni yake ina umbo kama "S". Kina ya wastani ni mita 3,332; kina kikubwa katika mfereji wa Puerto Rico kinafikia mita 8,605. Upana wa bahari ni kati ya km 2,648 kati ya Brazil na Liberia hadi km 4,830 kati ya Marekani na Afrika ya Kaskazini.
 
Kuna ghuba nyingi pamoja na bahari za pembeni. Atlantiki inabadilishana maji yake na Pasifiki na Bahari Hindi hasa kusini ya mabara ya Afrika na Amerika ya Kusini.
 
Jiografia ya Atlantiki

Atlantiki inafunika sehemu za mabamba ya gandunia ya Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini, Karibi, Afrika na Ulaya-Asia. Yanapokutana katika ya beseni uko mgongo kati wa Atlantiki ambao ni safu ya milima chini ya bahari. Mahali pachache inafikia hadi uwiano wa bahari na kuonekana kama visiwa.
 
Visiwa na funguvisiwa za Atlantiki
Visiwa vikubwa ni (vyenye alama ya * ni sehemu ya safu ya mgongo kati wa Atlantiki):

Greenland, *Iceland, Britania (Uingereza), Ueire (Ireland), Kuba, Newfoundland
 
Funguvisiwa muhimu ni: visiwa vya Faroe, visiwa vya *Azori, visiwa vya Madeira, visiwa vya Kanari, visiwa vya Cabo Verde, visiwa vya Karibi (pamoja na Kuba), visiwa vya Britania (pamoja na Uingereza na Ueire - Ireland, visiwa vya *Bermudas na vingine.
 
Funguvisiwa muhimu ni: visiwa vya Faroe, visiwa vya *Azori, visiwa vya Madeira, visiwa vya Kanari, visiwa vya Cabo Verde, visiwa vya Karibi (pamoja na Kuba), visiwa vya Britania (pamoja na Uingereza na Ueire - Ireland, visiwa vya *Bermudas na vingine.
 
Mikondo ya bahari
Mikondo ya Atlantiki inatawala hali ya hewa katika nchi zinazoongozana bahari. Kati ya mikondo hizi ni mkondo wa ghuba la Mexiko kutoka eneo la visiwa vya Karibi ukivuka Atlantiki na kubeba maji ya moto (ambayo bado ni vuguvugu kiasi wakati wa baridi) hadi pwani la Ulaya.
 
Back
Top Bottom