Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuchanyika ni ndege wadogo wa familia Cettiidae. Spishi za Erythrocercus zinaitwa ndwindwi au dwidwi. Ndege hawa wanafanana na shoro, kucha na kuchamsitu, na zamani wote waliainishwa pamoja katika familia Sylviidae. Spishi nyingine za kuchanyika zina mkia mrefu, nyingine zina mkia mfupi sana. Zina rangi ya kahawia au kijivu mgongoni na nyeupe au njano chini; spishi kadhaa zina rangi kali (Tesia k.m.). Spishi za Cettia tu zinatokea Ulaya, nyingine zinatokea misitu ya Afrika na Asia. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa kigoga, nyuzinyuzi, mizizi na/au majani. Jike huyataga mayai 2-6.
 
Ndwindwi au dwidwi ni ndege wadogo wa jenasi Erythrocercus katika familia Cettiidae. Spishi nyingine za familia hii zinaitwa kuchanyika. Ndwindwi wanafanana na chechele, lakini bila mkia mrefu sana, na kwa hivyo zamani waliainishwa katika familia Monarchidae. Jina la jenasi linatoka lugha ya Kiyunani: ερυθρος = nyekundu na κερκος = mkia. Mbili baina ya spishi tatu zina mkia mwekundu kwa kweli lakini ile ya tatu ina mkia njano. Ndwindwi wanatokea misitu ya Afrika kusini kwa Sahara. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa majani na malaika. Jike huyataga mayai 2-4.
 
Kuchanyika ni ndege wadogo wa familia Cettiidae. Spishi za Erythrocercus zinaitwa ndwindwi au dwidwi. Ndege hawa wanafanana na shoro, kucha na kuchamsitu, na zamani wote waliainishwa pamoja katika familia Sylviidae. Spishi nyingine za kuchanyika zina mkia mrefu, nyingine zina mkia mfupi sana
 
Zina rangi ya kahawia au kijivu mgongoni na nyeupe au njano chini; spishi kadhaa zina rangi kali (Tesia k.m.). Spishi za Cettia tu zinatokea Ulaya, nyingine zinatokea misitu ya Afrika na Asia. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa kigoga, nyuzinyuzi, mizizi na/au majani. Jike huyataga mayai 2-6.
 
Washonaji ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Cisticolidae. Wamepewa jina hili kwa sababu ndege hawa huunganisha majani kwa kushona na kutengeneza tago lao ndani yao. Wana mkia mrefu uwekwao juu mara nyingi. Rangi yao ni kahawia, kijivu au kijani mgongoni na nyeupe, njano au kijivu isiyokolea chini; spishi kadhaa zina utosi mwekundu
 
Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara na Asia ya tropiki katika misitu na mapori. Hula wadudu. Hulitengeneza tago kwa manyasi ndani ya majani yaliyoshonwa katika kichaka, mmea au kishungi cha manyasi. Jike huyataga mayai 2-3.
 
Korobindo ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Ploceidae. Kuna ndege wengine ambao wanaitwa korobindo katika familia Passeridae. Spishi hizi zinatokea Afrika tu
 
Ndege hawa wanafanana na shomoro lakini wana mwenendo kama kwera. Wana rangi ya kahawa au kijivu juu na nyeupe chini. Hula mbegu hasa na beri na wadudu pia.
 
Spishi hizi hulijenga tago lao ndani ya msongo wa manyasi na pengine vijitu pia ambao umebandikiwa tawi la mti. Korobindo mpendakundi hujenga jengo kubwa la manyasi linaloweza kuwa na nafasi kwa matago zaidi ya 100. Majengo haya yapo katika miti au juu ya nguzo zilizowekwa na watu kama vile nguzo za umeme. Jike huyataga mayai 3-5.
 
Kuchamsitu ni ndege wadogo wa familia Phylloscopidae. Wanafanana na shoro, kucha na kuchanyika, na zamani wote waliainishwa pamoja katika familia Sylviidae. Spishi za Phylloscopus zina rangi ya kahawia au kijani mgongoni na nyeupe au njano chini. Zile za Seicercus zina rangi kali zaidi, kijani mgongoni na njano chini
 
zina milia kichwani na mviringo wa jicho mweupe au njano. Ndege hawa wanatokea misitu ya Afrika, Asia na Ulaya. Spishi zinazozaa katika kanda za halijoto ya wastani huhamia kusi, zile za Ulaya huenda Afrika. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe ndani ya uoto mzito, mara nyingi karibu na ardhi. Jike huyataga mayai 2-7.
 
Magamaga ni ndege wadogo wa jenasi mbalimbali katika familia Cisticolidae. Wanafanana na videnenda lakini mkia wao ni mrefu zaidi na hawana michirizi mizito. Karibu na nusu ya spishi za Prinia zinatokea Asia lakini spishi zote nyingine zinatokea Afrika. Hawa ni ndege wa maeneo wazi yenye manyasi marefu na vichaka. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe ndani ya manyasi au kichaka karibu na ardhi; mara nyingi tago limefunika. Jike huyataga mayai 2-5.
 
Chozi ni ndege wadogo wa familia Nectariniidae. Spishi za jenasi kadhaa zinaitwa neli. Spishi nyingi sana zina rangi kali zinazong'aa juani kama metali. Manyoya ya kati ya mkia ni marefu sana katika spishi nyingine.
 
Domo lao limepindika na hutumika kwa kutoa mbochi katika maua au wadudu katika matundu. Hula mbochi hasa na pengine maji ya matunda na wadudu pia. Wawindaji-buibui, ambao wamo pia katika familia hii, hula wadudu zaidi kuliko chozi.
 
Ndege hawa wanatokea kanda za tropiki na nusutropiki za Afrika, Asia na kaskazini mwa Australia. Tundu lao lina umbo la mfuko na limening'izika kwa vitawi vyembamba. Jike hutaga mayai 2-4.
 
Njiri ni ndege wadogo wa jenasi Nesocharis, Nigrita na Parmoptila katika familia Estrildidae ambao wanatokea Afrika tu. Wanafana na mishigi wenye rangi za nyeusi, kijivu na kahawia, pengine nyekundu au buluu. Hula wadudu, matunda madogo na mbegu. Tago lao ni tufe la manyasi, nyuzinyuzi na vigoga lenye mwingilio kwa kando. Jike huyataga mayai 3-6.
 
Mbweta ni ndege wakubwa kiasi wa jenasi Chlorophoneus, Malaconotus na Telophorus katika familia Malaconotidae. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Ndege hawa wana rangi kali kwenye kidari na tumbo, k.m. nyekundu, machungwa, njano au kijani. Mgongo wao ni rangi ya majani au zeituni kwa kawaida. Wana domo nene lenye ncha kwa kulabu. Hula wadudu hasa na vertebrata wadogo pia, mijusi kwa kawaida. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe mtini na jike huyataga mayai 2-4.
 
Mlali au sekini ni ndege wa jenasi Prionops, jenasi pekee ya familia Prionopidae. Wanatokea Afrika kusini kwa Sahara tu. Spishi za Asia ambazo ziliainishwa katika familia hii, zimehamishwa ndani ya familia Tephrodornithidae. Mlali ni weusi na weupe, weusi na rangi ya kijivu au weusi, weupe na rangi ya kijivu pengine pamoja na rangi ya kahawianyekundu kwa tumbo.
 
Domo lao lina ncha kwa kulabu na rangi ya nyeusi au nyekundu; miguu ni myekundu mara nyingi. Ndege hawa wana ngozi yenye rangi kali (nyekundu au pinki) kuzunguka macho na ushungi kwa umbo wa helmeti wenye rangi ya nyeupe, kijivu, nyeusi au manjano. Hula wadudu na vertebrata wadogo. Hulijenga tago lao kwa vipande vya gome na tandabui mtini au kichakani na jike huyataga mayai 2-5.
 
Back
Top Bottom