Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

27575823_219942818553330_7695781379463708672_n.jpg
 
Wafanyabiashara wenye asili ya weupe walijaribu kumtumikia Bwana Ramaphosa ambae alipata hisa katika karibu kila sekta muhimu - kutoka kwa simu na vyombo vya habari (ambako hakuingilia kati katika uhuru wa wahariri wa magazeti ambayo alikuwa nayo) kwa vinywaji na chakula cha haraka alikuwa anaendesha msururu wa hoteli ya Marekani McDonalds nchini Afrika kusini.
 
Vibaraka wa kigeni

Bw Ramaphosa daima aliendelea kukiendeleza chama ANC, akiwa kiongozi mkuu wa kamati ya utendaji ya Taifa - nafasi ambayo, wakosoaji wake wanasema ilimpa habari za ndani na akiwa muhudumu wa serikali alitumia nafasi hiyo ya utawala wake kujijenga kibiashara.
 
Cyril Ramaphosa kwa kumtupia jicho:
1:Alizaliwa Soweto, Johannesburg, mwaka 1952
2:Mwaka 1974 mpaka 1976 aliwekwa kizuizini kwa shughuli za kupambana na ubaguzi wa rangi.
3:Alianzisha muungano wa kitaifa wa wafanyakazi wa migodi 1982
4:Mwenyekiti wa kamati ya mapokezi ya taifa yaliyoandaa kumpokea Nelson Mandela kutoka gerezani 1990
5:Mbunge na mwenyekiti wa mkutano wa kikatiba wa mwaka 1994
6:Mwaka 1997 aliamua kuingilia kikamilifu biashara kwa muda wote na kuwa moja wa matajiri wakubwa nchini Afrika kusini
7:Alikuwa Katika bodi ya Lonmin wakati wa mauaji ya wachimba mgodi wa Marikana 2012
8:2017 alichaguliwa kuwa kiongozi wa chama cha ANC
 
Back
Top Bottom