Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa mujibu wa ushahidi wa PW3 inaonekana tumeletewa kitu kingine kabisa leo,” alidai Magafu, kauli ambayo ilimnyanyua wakili wa Serikali mkuu, Peter Maugo, akipinga hoja hiyo.

Maugo alidai anachokifanya msomi mwenzake ni kufanya mlinganisho wa ushahidi wa mashahidi, jambo alilodai kwa hatua waliopo si sahihi bali ilipaswa ifanywe wakati wa majumuisho ya kesi.
 
Hata hivyo, Magafu alidai wanachobishania ni uhalali wa kielelezo kinachoombewa kipokewe na mahakama kwa utambuzi kwa vile kinatofautiana na kilichotambuliwa na PW3.

“Tarehe 6/10/2015 tuliletewa koti zima wakati shahidi wa tatu anatoa ushahidi wake. Leo tunaletewa koti lililokatwakatwa. Hii ndiyo hoja yetu,” alisisitiza Magafu na Jaji akamruhusu alizungumzie.
 
Hata hivyo, akijibu hoja hizo, wakili wa Serikali mwandamizi, Abdallah Chavula alidai hoja za mawakili wa utetezi zimewahishwa (premature) kwa vile upande wa mashtaka haujafunga kesi yake. “Prosecution (upande wa mashtaka) hatujafunga kesi na huyu shahidi sio wa mwisho, hivyo kuiaminisha mahakama kwa kuegemea ushahidi wa PW3 na PW9 si sahihi,” alieleza Chavula na kuongeza:
 
Wenzetu wanasema shahidi wa tatu alipolitambua jaketi lilikuwa halijakatwa na kinacholetwa leo (jana) ni tofauti, sisi tunasema si sahihi wala kumbukumbu ya hicho kitu haipo.”

Alidai siku alipotoa ushahidi wake, shahidi wa tatu alieleza tu ataweza kulitambua jaketi hilo kwa rangi yake na hakuna kumbukumbu za mahakama kuwa alilikagua.
 
Hata wakati analitambua (shahidi wa tatu) hapa mahakamani, hakulikagua huko ndani. Alionyeshwa jaketi kwa nje kwa ujumla wake akasema analitambua kwa rangi ya kaki.

“Hoja zinazoibuka leo kuwa sio lile, hazina mashiko wala mantiki. Kesi inaendelea na tuna mashahidi 50 na huyu leo ni wa 25 nani kasema hatakuja shahidi mwingine kulikabidhi?” Alihoji.

Akitoa uamuzi wake mdogo, Jaji Maghimbi alikubaliana na hoja za mawakili wa Serikali na kueleza kuwa anachokitolea ushahidi ni kile alicholetewa kukifanyia kazi.
 
Hata wakati analitambua (shahidi wa tatu) hapa mahakamani, hakulikagua huko ndani. Alionyeshwa jaketi kwa nje kwa ujumla wake akasema analitambua kwa rangi ya kaki.

“Hoja zinazoibuka leo kuwa sio lile, hazina mashiko wala mantiki. Kesi inaendelea na tuna mashahidi 50 na huyu leo ni wa 25 nani kasema hatakuja shahidi mwingine kulikabidhi?” Alihoji.

Akitoa uamuzi wake mdogo, Jaji Maghimbi alikubaliana na hoja za mawakili wa Serikali na kueleza kuwa anachokitolea ushahidi ni kile alicholetewa kukifanyia kazi.
 
Alichokisema shahidi ni kwamba alichokipata kutoka maabara ya Arusha ni mfuko ambao ndani yake kulikuwa na sampuli. Tunawezaje kutenganisha jaketi na sampuli alizozipokea pamoja?” Alihoji Jaji.

Jaji Maghimbi alilikataa pingamizi la mawakili wa utetezi na kukubali jaketi hilo lipokelewe kwa utambuzi, hivyo wakili Magafu akapata fursa ya kumhoji shahidi kuhusiana na ushahidi wake.

Alipoulizwa aliyemtajia majina yanayoonekana katika sampuli alizozipokea, shahidi huyo alidai majina hayo yalikuwapo katika nyaraka za utambuzi zilizowasilishwa kwake na RCO.

Magafu alimuuliza shahidi huyo kama anafahamu sampuli za damu na mate za washtakiwa hao eneo (place) zilikochukuliwa, alisema yeye hafahamu.

Kuhusu kama aliwahi kuletewa washtakiwa hao ili achukue upya sampuli za damu na mate, shahidi huyo alisisitiza kuwa sampuli alizoletewa alipelekewa na ofisi ya RCO Kilimanjaro.

Magafu alimuuliza shahidi huyo kuwa anazungumziaje kauli ya wateja wake (washtakiwa) wanaosema hawakuwahi kuchukuliwa mate wala damu, yeye alisema hajui.

Kesi hiyo inayovuta hisia za wengi inawakabili washtakiwa saba ambao ni Sharifu Mohamed, Shaibu Jumanne, Mussa Mangu, Jalila Zuberi, Karim Kihundwa, Sadick Jabir na Ally Mussa.
 
7B27446D-D8F3-4660-8D16-C7922742C395.jpeg
 
Back
Top Bottom