Kwa zaidi ya miaka 60 inakadiriwa kuwa amehubiri kwa jumla ya watu milioni 210.
Alikuwa Mkristo akiwa na umri wa miaka 16 baada ya kumsikiliza mhubiri mmoja na kuanza huduma ya mahubiri mwaka 1939.
Graham, ambaye alifanya kazi kama afisa wa mauzo, aliendelea na kuwa mmoja wa wahubiri wenye ushawishi mkubwa miongoni mwa watu wa dini zote huku akiwashauri marais na viongozi wengine wengi duniani juu ya imani ya Kikristo.
Mwaka 1949, alipata umaarufu wakati alihubiri kwa wiki nane kwenye hema kubwa huko Los Angeles.
Wakati wa harakati za mashirika ya kupigania haki za binadamu, Graham aliibuka kuwa mkasoaji mkubwa wa ubaguzi wa rangi nchini Marekani.
Ni muhubiri aliyeepuka kashfa mbalimbali zilizowazonga wahubiri wengi waliotumia runinga kusambaza injili.
Alijenga uhusiano wa kirafiki na marais kadhaa wa Marekani kuanziaTruman hadi Nixon na hata Obama. Mkutano wake wa mwisho wa hadhara ulikuwa mwaka 2005 jijini New York Marekani akiwa na umri wa miaka 86.
Rais Donald Trump amemuelezea Graham kama "mwanaume wa kipekee".
Akiandika kwenye ukurasa wake wa Twitter, Trump amesema "Mhubiri maarufu wa Injili Billy Graham. Hakuna aliyekuwa kama yeye! Atakumbukwa na Wakristo na watu wa dini zote. Mwanamume wa kipekee kabisa."
Wakazi wa kijiji cha Colombia cha Quinamayó wamekua wakisherehekea Krismasi wakiwa na sa namu ya mtoto Yesu mweusi
Wanakijiji wanasema kuwa uitamaduni huu ambao ulianza tangu enzi za utumwa wakati mababu zao walipozuiwa kusherehekea Krismasi tarehe 24 Disemba.
Badala yake waliamua kuchagua katikati mwa mwezi wa Februari na utamaduni huu umeendelea tangu wakati huo.
Fataki, muziki na densi huwa sehemu ya sherehe hizo za kuvutia.
"Watu waliotufanya watumwa walisherehekea Krismas Disemba na hatukuruhusiwa kuwa na mapumziko siku hiyo, lakini tukaambiwa tuchague siku nyingine," alisema, Holmes Larrahondo, mratibu wa sherehe.
Katika jamii yetu tunaamini kwamba mwanamke anapaswa kufunga siku 45 baada ya kujifungua, kwa hiyo tunasherehekea Krismas sio mwezi Disemba, bali Februari, kwa hiyo Maria anaweza kudensi pamoja nasi," aliongeza Bw. Larrahondo.
Katika jamii yetu tunaamini kwamba mwanamke anapaswa kufunga siku 45 baada ya kujifungua, kwa hiyo tunasherehekea Krismas sio mwezi Disemba, bali Februari, kwa hiyo Maria anaweza kudensi pamoja nasi," aliongeza Bw. Larrahondo.
Balmores Viafara, mwalimu mwenye umri wa miaka 53 aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba kutokana na hilo kwake tarehe 24 Disemba "ni kama siku nyingine yoyote ile "
Wakati wa kuabudu, sherehe hizo huitwa "sherehe za kutoa heshma kwa Mungu wetu kwa namna yetu."
Kama sehemu ya sherehe hizi, wanakijiji hutembelea nyumba mbali mbali "wakimtafuta mtoto Yesu', ambaye huwakilishwa na sanamu ya mbao ambayo hutunzwa na mmoja wa wanavijiji katika nyumbani kwake kwa kwa kipindi cha mwaka kilichosalia.
Pale sanamu inapopatikana, hutembezwa kijijini na wakazi wa rika zote waliovalia kama malaika na wanajeshi.
Wacheza densi, hucheza densi inayoitwa fuga; ambapo hucheza wakiigiza hatua za watumwa waliofungwa minyororo.
Sherehe humalizika majira ya asubuhi mapema.
Mvinyo mwekundu awali ulihusishwa na faida mbali mbali za kiafya, kuanzia kusaidia kupunguza kihatari za kupata magonjwa ya moyo na na kisukari.
Sasa utafiti mpya unasema mvinyo huu una kemikali ambazo zinakabiliana na kuoza kwa meno na ugonjwa ufizi.
Watafiti walibaini kuwa mchanganyiko wa kemikali unaotengeneza kinywaji hicho, unaofahamika kama polyphenols, husaidia kumaliza kuwamaliza vimelea (bakteria) hatari kinywani.
Lakini watafiti hawa wanaonya kuwa matokeo ya utafiti wao hayatoi "ruhusa'' ya kunywa mvinyo kupita kiasi.
Utafiti wa awali ulionnyesha kuwa faida za kiafya za polyphenols zilihusishwa na kuwa na uwezo wa kuulinda mwili dhidi ya vimelea hatari wanaoshambulia mwili.
Hata hivyo, utafiti wa hivi karibuni umeonyesha kuwa kemikali salama ya polyphenols inaweza kuboresha afya kwa kufanya kazi na "vimelea wazuri " katika tumbo zetu.
Katika utafitihuu uliochapishwa katika jarida la Kemikali za Kilimo na Chakula , wanasayansi walichunguza ikiwa kemikali ya mvinyo ya polyphenols inaweza pia kuwa nzuri kwa afya ya kinywa.
Watafiti walilinganisha athari za aina mbili za kemikali ya polyphenols kutoka kwa mvinyo mwekundu dhidi ya mbegu ya zabibu na kiasi kidogo cha mvinyo mbadala kwenye bakteria wanaoganda kwenye ufizi na meno na kusababisha magonjwa ya kinywa, kuoza kwa meno naugonjwa wa ufizi.
Walibaini kuwa kemikali ya mvinyo na mvinyo kwa pamoja vilipunguza uwezo wa Bakteria wa kukaa kwenye seli, lakini kemikali zaa polyphenols - caffeic na p-coumaric acids - zilifanya kazi bora zaidi .
Mvinyo mwekundu una kiwango kikubwa cha kemikali za polyphenols, lakini pia zinaweza kupatikana katika machungwa na vinywaji na vyakula vifuatavyo:
Vinywaji:
Kahawa
Chai ya majani chai mabichi
Chai ya kawaida ya majani
Maji ya matunda tufaha
Maji ya machungwa na limao
Katika vyakula hupatikana katika:
madini ya bluberi
maharagwe
Zabibu nyeusi
Nyota wa muziki wa pop nchini Marekani Madonna amesema kuwa mwanawe David Banda atakuwa rais wa Malawi siku zijazo katika ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa Twitter akimsifu mvulana huyo mwenye umri wa miaka 12.
Mwanamuziki huyo wa Marekani ana watoto sita ,wanne akiwa aliwahasili kutoka Malawi. Madonna amekuwa na uhusiano mbaya na mamlaka ya taifa hilo la kusini mashariki mwa Afrika.
Mwaka 2013 Malawi ilimshutumu Madonna kwa kutumia ushawishi wake kuwatishia maafisa wa serikali akisisitiza mchango wake kwa taifa hilo mbali na kutaka kupewa heshima.
Meneja wa Madonna aliishutumu serikali ya Malawi kwa kiuwa na chuki dhidi ya shirika la hisani la nyota huyo la Raising Malawi ambalo alilianzisha 2006 mwaka huohuo aliomuasili David.
Ruka ujumbe wa Twitter wa Madonna
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.