Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

18157CC3-2C1C-4694-9D41-F59E549CDB4B.jpeg
 
KATIKA mkutano mkubwa wa hadhara, bwana mmoja aliyekuwa amesimama katikati ya umati wa wahudhuriaji, alitoa bango kubwa (pana na refu) na kulinyanyua juu akilielekeza jukwaa kuu (mbele). Bango hilo kubwa liliwakera waliosimama nyuma yake, kwa sababu kwanza liliwakinga, na pili hawakuweza kuusoma ujumbe ulioandikwa kwa mbele. Na waliosimama mbele ya jamaa huyo, pia hawakutambua kama kuna mtu nyuma yao amenyayua bango lenye ujumbe f'lani. . Kwa bahati, viongozi walioketi meza kuu ndiyo waliliona vizuri bango hilo na kuusoma ujumbe wake. Kwa ujumbe ule, wapo waliocheka na wapo waliostaajabu. Hali hiyo, ikawafanya waliosimama mbele ya jamaa, kugeuka nyuma na kusoma kilichoandikwa. Nao, kama ilivyokuwa kwa wale wa meza kuu, walicheka ilhali baadhi yao wakistaajabu. Haikuwa rahisi kwa waliosimama nyuma kwenda mbele ya jamaa ili kuusoma ujumbe, hivyo waliendelea kusimama bila ya kujua kilichoandikwa huku wakipata taabu ya kukingwa na bango hilo. . Bango lilisomeka hivi: NIMENYANYUA HILI BANGO ILI TU KUWAKINGA WALIO NYUMA!. . Na kwenye maisha kuna watu wako vivyohivyo wankuwekea bango kubwa maishani ili kukuzuia, bila sababu ya msingi, usifanikiwe. Usipojiongeza hutafanikiwa na hutagundua kama umekingwa na bango kubwa ajabu.
Kuna mabango mengi maishani ingawa inchi kama Tanzania imewekewa mabango mengi ya aina hiyo, ingawa miongoni mwetu hudhani mabango hayo ni kivuli tu toka kwa mataifa yanayo tupenda
 
Wametumia

Wametumia mbinu gani kuupata utajiri huo wa Mansa K. Mussa
Yaani sielewi kabisa!
Alafu wadhungu walivyo wajanja wakaifanya nchi ya Mali ionekane dhaifu kuliko nchi zote duniani!
Mji mkuu wa Mali,Timbuktu, Hollywood ndiyo wanautumia kama HELL LIKE PLACE!
Ukiangalia deep GHADAFI aliijua hiyo Siri maana vitu alivyofanya nchini kwake kwa kweli ni vya ajabu!
Hata na Omani nako pia...,,
Mansa K Mussa ni trading na Ghadafi ilikuwa Oil!
 
Back
Top Bottom